Chama cha Skauti kina mengi ya kurekebisha
|
Mlezi wa Skauti Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete (Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mlezi wa Skauti Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajia kumwapisha Skauti Mkuu mteule ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mh. Mwantum Mahiza, taarifa iliyotufikia kutoka kwa mtoa taarifa wetu inasema, tarehe 19 Juni, 2013 Skauti Mkuu mteule ataapishwa na kufuatiwa na shamra shamra katika viwanja vya Karimjee siku hiyo hiyo.
Katika hatua nyingine Skauti Mkuu atakutana na changamoto nyingi za migogoro ndani ya Chama cha Skauti Tanzania. Baadhi yake ni pamoja na migogoro ya umiliki wa ardhi ambao unawahusu wadhamini wa chama katika kesi namba 185/2004 katika Mahakama Kuu ya Tanzania, katka kesi hii inasadikiwa waliokuwa viongozi miaka ya 2003 waliingia mikataba isiyofuata taratibu kwa mujibu wa katiba ya chama cha Skauti Tanzania. Kwa upande wa kesi hii ambayo iliyochukua muda mrefu sana, Chama cha Skauti kimeshindwa kutafuta suruhisho nje ya Mahakama hii inatokana na baadhi ya viongozi wa Skauti kutoifuatilia, athali yake itapelekea wadhamini wa Chama cha Skauti kupandishwa Mahakamani. Kesi hii itasikilizwa tena tarehe 06 Juni, 2013 katika Mahakama Kuu ya Tanzania.
|
Mh. Mwantum Mahiza Skauti Mkuu Mteule (Mkuu wa Mkoa wa Pwani) |
Kwa upande mwingine, kesi ya kukamatwa na kutaka kuuzwa kwa jengo la chama cha Skauti ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa hukumu ya Mahakama kuu ya Kazi Tanzania ni madai ya msingi ya Bi. Agnes George. Katika kesi hii yenye namba 175/2009, Chama cha Skauti kikiwa na dai moja wapo la msingi kuwa Bi. Agnes anakidai chama kiasi cha Tsh 5,300,385.60 na kwa upande wa mdai ana hoja yake ya msingi ya madai ya Tsh 111,510,384.60. Ikumbukwe pia katika kesi hii ilikwisha kipelekea Chama kukamatwa na kuuzwa kwa gari aina ya Suzuki - Vitara ikiwa kama fidia ya mdaiwa. Kesi hii imepangwa kusikilizwa tarehe 20 Juni, 2013 katika Mahakama Kuu ya Tanzania.
Mbali na matatizo au chanagamoto hizo ambazo Skauti Mkuu na uongozi wake unaotarajiwa unahitaji kuzimaliza kwa haraka zaidi ukizingatia ni za muda mrefu. Pia chama kimepoteza mvuto kwa jamii na kuwa na makundi, mikataba isiyokuwa na tija, karakana ya kutengenezea magari (Garage), sehemu ya kuuzia vileo (Bar) na ujenzi holela katika eneo la makao makuu ya Skauti ambayo upelekea kuchafua sura na mandhari ya eneo.