Ijumaa, 31 Mei 2013

FOMU YA MAFUNZO YA PTC NA WOOD BADGE



Fomu ya kushiriki Mafunzo ya Awali ya Uongozi (PTC)

Fomu ya Kushiriki Mafunzo ya "WOOD BADGE"


Watu  wazima wanaopenda Skauti na Skauti wenye umri kuanzia miaka 18 ambao hawajapata mafunzo ya uongozi ya awali wanayo nafasi ya kushiriki mafunzo haya. mafunzo ya Awali (PTC) yataanza tarehe 13 mpaka 16 mwezi wa Juni, 2013. Na mafunzo ya WOOD BADGE yataanza tarehe 15 mpaka 25 mwezi Juni, 2013. Fomu za kushiriki mafunzo hayo zinapatikana sasa.
Kwa zaida tembelea: http://www.facebook.com/groups/171718552973513/

Jumatatu, 27 Mei 2013

Mafunzo ya PTC na Wood Badge

Kamishna Abubakari Mtitu
Chama cha Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam kimeandaa mafunzo ya awali ya uongozi kwa Skauti. Hii ni fursa kwa Skauti kuanzia miaka ya 18 na kuendelea kupata mafunzo hayo.

Kwa mujibu wa Kamishna Skauti mkoa wa Dar Es Salaam, Kamishna Abubakari Mtitu alisema, Mafunzo hayo ni fursa kwa watu wazima kujifunza Skauti na ata wale walio mikoa mingine wanakaribishwa kushiriki mafunzo.
Kamishna Mtitu aliongeza kusema, "Tumeandaa fursa nyingine ya mafunzo ya watu wazima katika ngazi ya Wood Badge ili tuweze kupata watu wazima watakaoweza kusimamia shughuli za Skauti katika ngazi mbalimbali".

Kwa wale watakaopenda kushiriki mafunzo hayo, fomu za ushiriki zinapatikana sasa, tafadhali pakua fomu hizo kwa kubonyeza hapa; http://www.facebook.com/groups/171718552973513/

Jumamosi, 18 Mei 2013

TANZIA TANZIA TANZIA

Maskauti wakiwa wamezunguka Sanduku la Marehemu Emmanuel Peter Ndungwi wakiwa katika Kanisa Katoriki, Tegeta katika Misa ya kumuombea marehemu tarehe10 Mei, 2013

Marehemu Emmanuel Peter













Chama cha Skauti Tanzania kimepata msiba wa mwanachama wake Marehemu Skauti Emmanuel Peter Ndungwi aliyefariki tarehe 9 Mei, 2013 katika hospitali ya Temeke Dar Es Salaam, Kwa mujibu wa taarifa ya kiongozi wake wa kundi la Skauti la St. Mary Morogoro Skauta Omari Juma alisema, Marehemu Emmanuel alizaliwa tarehe 22 Aprili, 1999 uko Dodoma na kusoma katika shule ya msingi St. Mary's mkoani Morogoro hadi kifo kinamfikia akiwa darasa la sita.

WASIFU WA MAREHEMU

Kwa mujibu wa dada wa marehemu Bi. Veronica Ndungwi amesema, marehemu Emmanuel alibatizwa mwaka 2003 mkoani Kigoma katika Parokia ya Mt. Ceccilia, alipata Komonio ya kwanza pamoja na Kipa Imara mwaka 2012 katika Parokia ya Kihonda Mkoani Morogoro. Marehemu alitumikia Kanisa kama muhudumu wa Altare ya bwana.
Marehemu alijiunga na Skauti tarehe 14 Machi, 2011 hadi anafariki alikuwa mwanachama wa Skauti. Alishiriki katika kambi na mafunzo mbalimbali na kambi yake ya mwisho ilikuwa tarehe 13 hadi 16 Februari 2013 iliyofanyika katika Kambi la Taifa ya Skauti (BAHATI CAMP) Mjini Morogoro .

Marehemu Emmanuel alianza kuumwa tarehe 29 Aprili, 2013 na alifariki tarehe 9 Mei, 2013 katika hospitali ya Temeke jijini Dar Es Salaam baada ya kuugua ugonjwa wa Maralia na Homa ya matumbo (Taifodi)

Jumanne, 14 Mei 2013

MAOMBI YA NAFASI YA KAMISHINA MKUU

Chama cha SKAUTI Tanzania kinakaribisha maombi ya kugombea nafasi ya KAMISHINA MKUU.
Katika kikao chake cha Viongozi waandamizi (Skauti Mkuu, Kamati Tendaji, Kamati ya Mpito na Wakufunzi) kilichofanyika tarehe 09 Mei, 2013 chini ya Uenyekiti wa Skauti Mkuu Mh. Mwantum Mahiza kimeazimia mambo yamsingi yafuatayo:-

  • ·     Kutangaza kimaandishi nafasi iliyowazi ya Kamishna Mkuu.  Hii ni nyongeza ya tangazo alilolitoa Skauti Mkuu katika Mkutano wake na viongozi mbali mbali jijini Dar es Salaam uliofanyika tarehe 06 Mei 2013.
  • ·    Kutoa sifa na fomu za kugombea.

Sifa na Fomu za kugombea nafasi hiyo zinatolewa Makao Makuu ya Chama kuanzia tarehe 10 Mei, 2013.   
Pia zinapatikana katika www.DaresSalaamlocalscout.blogspot.com Search Google: - Dar Es Salaam Local Scouts Association.  Fomu zinaweza kurejeshwa kwa njia zifuatazo:-

-      Kwa “Despatch” kwa Mwenyekiti au Karani wake, Makao Makuu ya Chama.
-      Kwa “Registered Mail – Mwenyekiti wa Kamati ya mpito, Chama cha Skauti Tanzania S.L.P 945 DSM.
-      Kwa E-mail:szone2012@live.com

Mwisho wa kurejesha fomu ni tarehe 20 Mei 2013, saa 10.00 jioni.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Mpito Brigedia Jenerali Mstaafu Gerald Mkude, ameelezea sifa za mwombaji wa nafasi hiyo ni:-
 
1.           Awe Kamishna au aliwahi kuwa Kamishna

2.           Awe Mtanzania

3.           Awe hajawahi kuachishwa uongozi katika Chama cha Skauti au kushitakiwa kwa makosa ya jinai kwa kipindi cha miaka minne (4) iliyopita.

4.           Awe ametunukiwa Nishani ya Skauta (Woodbadge Holder)

5.           Awe na Elimu ya Sekondari au zaidi.

6.           Awe na uzoefu wa uongozi na utawala katika shughuli za Skauti na jamii kwa ujumla kwa muda usiopungua miaka 5.

7.           Awe ametoa mchango mkubwa wa huduma kwa Chama cha Skauti na jamii kwa ujumla.

8.           Awe ana uwezo wa kusimamia, kulinda na kutetea Katiba na Kanuni za Skauti wakati wote.

9.           Awe mtu wa kujiamini na kujitambua.

10.       Awe mweledi na mwaminifu

11.       Awe na uwezo wa mawasiliano Kitaifa na kimataifa.

12.       Awe mwenye umri wa miaka 35 au zaidi

Mwombaji atajaza Fomu iliyotayarishwa, pia alete maelezo yake binafsi yaani C.V. yake.

Pamoja na hayo, fomu ya kugombea nafasi hiyo inapatikana kwa kiitroniki katika ukurasa wa Facebook wa Dar Es Salaam Scout, bonfya hapa: http://www.facebook.com/#!/groups/171718552973513/

Fomu hiyo ipo katik utaratibu ufuatao:-
 
FOMU YA KUGOMBEA NAFASI YA KAMISHNA MKUU

FOMU NO: …………..

SEHEMU (A): MAELEZO BINAFSI (HERUFI KUBWA)

1.  JINA KAMILI   ……………………………………………………………….
2.  UMRI   …………………...  MAKAZI ……………………………         
3.  ELIMU ………………………………………………………………………….
4.  KAZI    …………………………………  MAHALI  ………………………
5.  ANUANI YA POSTA    ……………………………………………………
6.  SIMU   ……………………  EMAIL  ………………………………………
  1. UZOEFU WA UONGOZI
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………

  1. SAHIHI ………………………………………………….
SEHEMU (B):      MAONI YA KIKAO CHA UCHAMBUZI
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………

SAHIHI YA MWENYEKITI/KATIBU……………………………….. TAREHE …………….

SEHEMU (C):      MATOKEO YA UCHAMBUZI
………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………

SAHIHI YA MWENYEKITI/KATIBU……………………………….. 
TAREHE ……………………

 
Mwisho wa kurejesha fomu ni tarehe 20 Mei 2013, saa 10.00 jioni.

Jumatano, 8 Mei 2013

MZEE MWINYI NA SALIM WANUSURU KUUZWA KWA JENGO LA SKAUTI

 Mzee Ali Hassan Mwinyi Mdhamini wa Skauti Tanznia (Rais Mstaafu wa Tanzania)

Wadhamini wa Chama cha Skauti Tanzania Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim (pia alikuwa Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika-OAU)  wameingilia kati katika hatua za kunusuru jengo la Skauti Makao Makuu  lililopo Upanga jijini Dar Es Salaam lisiuzwe kwa mnada  na Kampuni ya Madalali ya Flamingo kufuatia utekelezaji wa hukumu ya Mahakama ya Kazi.

Katika mahojiano na 'Chombo cha habari cha Skauti Dar Es Salaam' Mwenyekiti wa Kamati ya Mpito Brigedia Jenerali Mstaafu Gerald Mkude alibainisha kuwa, tarehe 28 Aprili, 2013 alipigiwa simu na msaadizi wa Mzee Mwinyi na kumtaka kuwepo na kikao cha dharura kati ya wadhamini wa chama pamoja na viongozi wa kamati zote mbili (kamati ya mpito ikiongozwa na Ndugu Mkude na kamati tendaji ikiongozwa na Balozi Kuhanga). "Nilitoa taarifa kwa wenzangu kwa kuwepo na kikao cha dharura na wadhamini wa chama na tarehe 29 Aprili, 2013 tulikaa kikao" alisema ndugu Mkude.
Ndugu Mkude alieleza kuwa katika kikao hicho wadhamini wa chama walihoji sababu zilizopelekea kukamatwa kwa jengo na kutaka kuuzwa kwa mnada ndani ya siku 14. "Niliwaelezea sababu hizo na kuwapa taarifa tulizozichukua kwa muda huo" alisema ndugu Mkude.
Pia katika kikao hicho wadhamini wa chama Rais Mstaafu Mzee Mwinyi na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim walizitaka kamati zote mbili kufuata taratibu za kisheria haraka kwa ajili ya zuio la mahakama kupisha hatua zaidi ya kunusuru jengo hilo.

Wakili wa kujitegemea kutoka katika Kampuni ya Mawakili ya APEX ATTORNEYS walipendekezwa katika mchakato wa kutetea kuuzwa kwa jengo la Skauti, tarehe 5 Mei, 2013 wakili wa Apex Attorneys na Mwenyekiti wa  Kamati ya Mpito Brigedia Jenerali Mstaafu Gerald Mkude walipitia mapendekezo na sababu za zuio (Stop Order) la kupinga hukumu ya mahakama ya kazi kukamata na kutaka kuuzwa kwa mnada jengo la Skauti Upanga Dar Es Salaam.
"Tarehe 6 Mei, 2013 wakili wetu alinitaarifu kuwa Mahakama Kuu imekubali ombi letu na hukumu inachapishwa" alisema Ndugu Mkude.
7 Mei, 2013 Msajili wa Mahakama Kuu aliridhia sababu za kutouzwa kwa jengo na kutaka pande zote mbili (mdai na mdaiwa) kukutana na kuafikiana madai halali ya malipo ya mdai Bi. Agnes George.

MAHESABU YATOFAUTIANA

Katika hali isiyo ya kawaida, baada ya kupitia makalablasha mawakili wanaokiwakilisha Chama cha Skauti Tanzania wabaini kiwango cha madai na hoja ya msingi anayodai Bi. Agnes George yanatofauti kubwa, yanakadiliwa kufikia Milioni tano Shilingi za Kitanzania tofauti na hoja yake ya msingi ya madai ya Tsh 111,510,384.60.

Brigedia Jenerali Mstaafu Ndugu Gerald Mkude Mwenyekiti wa Kamati ya Mpito.
Ndugu Mkude alieleza kuwa, kesi itasikilizwa tarehe 23 Mei, 2013 Mahakama Kuu ambapo upande wa mdai Bi. Agnes George na mdaiwa Skauti Tanzania watawasilisha maoni yao kuhusu uhalali wa madeni yao kwani upande wa mdai unahoja ya kudai 111,510,384.60 na mdaiwa ukiwa na hoja ya kudaiwa  kiasi kinachokadiriwa kutozidi Milioni Tano fedha za Kitanzania.
"Suala la mnada limesitishwa, ninawashukuru wadhamini wa chama kwa kutuongoza vyema, nawashukuru pia kamati zote mbili na wanachama wote wa Skauti kwa mchango wao wa hali na mali, utulivu, maombi na dua zao katika hali hii" alisema Ndugu Mkude na kuahidi kutoa ushirikiano na taarifa kwa wakati katika kipindi hichi.

HATI YA PINGAMIZI