Jumapili, 23 Februari 2014

SHEREHE ZA KUMBUKUMBU YA KUZALIWA BADEN-POWELL ZAFANA



MAKAMISHNA WA SKAUTI MIKOA NA NAIBU WAO WAAPISHWA

 

Sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mwasisi wa Skauti Duniani Marehemu Baden-Powell zimefanyika katika nchi mbalimbali za Dunia.
Katika Jiji la Dar Es Salaam Sherehe hizo zilifanyika katika Kiwanja cha Kimataifa cha Biashara cha Mwalim Julius Kambarage Nyerere (Saba-Saba) barabara ya kilwa.
Shughuli hiyo iliyoandaliwa na Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam kwa kamati iliyoongozwa na Kamishna wa Skauti wa Mkoa huo Ndugu Abubakar Mtitu.


Mgeni rasmi Bi. Consolata Mgimba (aliyevaa suti nyeusi) Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Ufundi, kwa niaba ya Rais wa Chama ambaye ni Waziri wa Elimu na Mafunzo Mheshimiwa Shukuru Kawambwa tayari akisubiria maandamano ya Skauti, kulia ni Kamishna Mkuu wa Skauti Mheshimiwa Abdulkarim Shah, akifuatiwa na Makamo Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Taifa Mzee Mwaking'inda (aliyevaa suti) na kushoto mwa picha ni Naibu Kamishna Mkuu ndugu Rashidi Mchatta. Tarehe 22 Februari 2014 kaika kiwanja cha kimataifa cha biashara cha Mwl. Nyerere Dar Es Salaam.

Katika sherehe hiyo, Kamishna Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania (TSA) ndugu Abdulkarim Ismail Shah aliwaapisha Kamishna wa Mikoa na Manaibu wake.
Pia katika sherehe hiyo chama cha Skauti Tanzania kilizindua Mpango Mkakati wa Chama hicho.

Mgeni wa rasmi katika Sherehe hiyo alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Ufundi Stadi Bi. Consolata Mgimba kwa niaba ya Rais wa Chama ambaye ni Waziri wa Elimu na Mafunzo Mheshimiwa Shukuru Kawambwa alifika katika eneo la sherehe mnamo saa nne asubuhi tayari kwa kupokea maanamano na kuaza kwa sherehe hiyo.

Mgeni rasmi Bi. Consolata Mgimba Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Ufundi akivishwa Skafu na Skauti tayari kupokea maandamano ya Skauti, tarehe 22 Februari 2014

Kamishna Mkuu wa Skauti Mheshimiwa Abdulkarim Shah, akizungumza baada ya salamu zake kwa siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Baden-Powell.
Tarehe 22 Februari 2014 kaika kiwanja cha maonyesho ya kimataifa ya biashara cha  Mwl. Nyerere Dar Es Salaam.

Mgeni rasmi Bi. Consolata Mgimba Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Ufundi akitoa salamu kwa niaba ya Rais wa Chama ambaye ni Waziri wa Elimu na Mafunzo Mheshimiwa Shukuru Kawambwa