Jumatano, 11 Juni 2014

WOODBADGE COURSE FORM 2014


Jumapili, 23 Februari 2014

SHEREHE ZA KUMBUKUMBU YA KUZALIWA BADEN-POWELL ZAFANA



MAKAMISHNA WA SKAUTI MIKOA NA NAIBU WAO WAAPISHWA

 

Sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mwasisi wa Skauti Duniani Marehemu Baden-Powell zimefanyika katika nchi mbalimbali za Dunia.
Katika Jiji la Dar Es Salaam Sherehe hizo zilifanyika katika Kiwanja cha Kimataifa cha Biashara cha Mwalim Julius Kambarage Nyerere (Saba-Saba) barabara ya kilwa.
Shughuli hiyo iliyoandaliwa na Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam kwa kamati iliyoongozwa na Kamishna wa Skauti wa Mkoa huo Ndugu Abubakar Mtitu.


Mgeni rasmi Bi. Consolata Mgimba (aliyevaa suti nyeusi) Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Ufundi, kwa niaba ya Rais wa Chama ambaye ni Waziri wa Elimu na Mafunzo Mheshimiwa Shukuru Kawambwa tayari akisubiria maandamano ya Skauti, kulia ni Kamishna Mkuu wa Skauti Mheshimiwa Abdulkarim Shah, akifuatiwa na Makamo Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Taifa Mzee Mwaking'inda (aliyevaa suti) na kushoto mwa picha ni Naibu Kamishna Mkuu ndugu Rashidi Mchatta. Tarehe 22 Februari 2014 kaika kiwanja cha kimataifa cha biashara cha Mwl. Nyerere Dar Es Salaam.

Katika sherehe hiyo, Kamishna Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania (TSA) ndugu Abdulkarim Ismail Shah aliwaapisha Kamishna wa Mikoa na Manaibu wake.
Pia katika sherehe hiyo chama cha Skauti Tanzania kilizindua Mpango Mkakati wa Chama hicho.

Mgeni wa rasmi katika Sherehe hiyo alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Ufundi Stadi Bi. Consolata Mgimba kwa niaba ya Rais wa Chama ambaye ni Waziri wa Elimu na Mafunzo Mheshimiwa Shukuru Kawambwa alifika katika eneo la sherehe mnamo saa nne asubuhi tayari kwa kupokea maanamano na kuaza kwa sherehe hiyo.

Mgeni rasmi Bi. Consolata Mgimba Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Ufundi akivishwa Skafu na Skauti tayari kupokea maandamano ya Skauti, tarehe 22 Februari 2014

Kamishna Mkuu wa Skauti Mheshimiwa Abdulkarim Shah, akizungumza baada ya salamu zake kwa siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Baden-Powell.
Tarehe 22 Februari 2014 kaika kiwanja cha maonyesho ya kimataifa ya biashara cha  Mwl. Nyerere Dar Es Salaam.

Mgeni rasmi Bi. Consolata Mgimba Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Ufundi akitoa salamu kwa niaba ya Rais wa Chama ambaye ni Waziri wa Elimu na Mafunzo Mheshimiwa Shukuru Kawambwa

Jumatano, 19 Februari 2014

RATIBA YA SHEREHE YA SIKU YA MWANZILISHI WA SKAUTI DUNIANI LORD BADEN POWEL - 22 FEBRUARI 2014



MUDA
TUKIO
MHUSIKA
Saa 3:00 Asubuhi
Skauti kuwasili Uwanja wa Taifa
Skauti wote
Saa 3:30 Asubuhi
Maandamano kuelekea viwanja vya Mwl. Nyerere, Saba Saba
Skauti na Viongozi wao
Saa 3:30 Asubuhi
Ø  Viongozi wa Chama kuwasili Ukumbini.
Ø  Skauti Mkuu na Mwenyekiti Kamati Tendaji(T)  kuwasili ukumbini.
Ø  Wageni waalikwa kuwasili ukumbini.
Kamati ya Mapokezi/ MC
Saa 4:00 Asubuhi
Mgeni Rasmi kuwasili Uwanjani na kuvishwa Skafu.
Ø  Mgeni Rasmi kupokea maandamano.
Kamishna Mkuu,
Naibu Kamishna Mkuu,
Kamishna wa Mkoa(DSM)
Kamishna Mtendaji,

Saa 4:05
Asubuhi
Mgeni Rasmi kuingia Ukumbini.
Ø  Wimbo maalum (Twamkumbuka Mzee wetu Baden Powell)
Ø  Utambulisho wa wageni maalum
Skauti wote


Kamishna Mkuu
Saa 4:15
Asubuhi
Nasaha za Skauti Mkuu
Skauti Mkuu
Saa 4:30 Asubuhi
Burudani
MC
Saa 4:40 Asubuhi
Uzinduzi wa Mpango Mkakati
(Strategic Plan 2014 – 2017)
Mgeni Rasmi,
Kamishna Mkuu Msaidizi Miradi.
Saa 4:50 Asubuhi
Kuapishwa kwa Makamishna wa Mikoa
Ø  Burudani.
Kamishna Mkuu
Skauti.
Saa 5:20 Asubuhi
Kuwekwa saini kwa Mkataba wa Hifadhi ya Msitu wa Vikindu
Kamishna Mkuu
Mkurugenzi wa Hifadhi ya Misitu
Saa 5:30 Asubuhi
Burudani (Maonesho ya Sanaa ya mapigano)
Kikosi cha Rova
Saa 5:40 Asubuhi
Tukio maalum

MC

Saa 5:50 Asubuhi
Nasaha za Mgeni Rasmi
Mgeni Rasmi
Saa 6:00 Mchana
Kurudia Ahadi
Wote/ Kamishna Mkoa
Saa 6:05 Mchana
Neno la shukrani
Mwenyekiti Kamati Tendaji
Saa 6:15 Mchana
Chakula
Kamati ya Chakula

MWISHO

Jumamosi, 18 Januari 2014

KAMATI YA UENDESHAJI YA MKOA YATEMA CHECHE


 Kuandaa Siku ya kumbukumbu ya Mwanzilishi wa Skauti Duniani

Mwenyekiti wa kikao cha Kamati ya Uendeshaji Mkoa wa Dar Es Salaam (aliyekaa mbele) Kamishna Abubakar Mtitu akiongoza ajenda katika kikao cha kamati hiyo tarehe 18 Januari katika Mgahawa Upanga Dar Es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Uendeshaji Mkoa wa Dar Es Salaam wakijadili ajenda katika kikao tarehe 18 Januari katika Mgahawa Upanga Dar Es Salaam.
Wa kwanza kushoto ni Mwanyato James, Titto Jackson, Bi Ramadevi na Naibu Kamishna Mkoa wa Dar Es Salaam Bi Grace Kado.

Chama cha Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam kupitia Kikao chake cha Kamati ya uendeshaji kimetoa wito kwa Skauti Mkoa wa Dar es Salaam kujiandaa na siku ya kumbukumbu ya mwanzilishi wa Skauti Duniani (Founder's Day) inayotarajiwa kufanyika kimkoa kuanzia tarehe 21 Februari, 2014 mpaka 23 Februari, 2014.
 
Kamishna wa Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam Ndugu Abubakar Mtitu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kikao cha kamati Uendeshaji cha Mkoa wa Dar Es Salaam, katika kiwanja cha Makao Makuu ya Skauti Upanga tarehe 18 Januari, 2014

"Wito unatolewa kufanya kazi za huduma kwa jamii kwa kujitolea kama ilivyo ada na wajibu wa Skauti" alisema Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Kamishna wa Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam Kamishna Abubakar Mtitu. Ndugu Mtitu alisisitiza kuwa Skauti ni watu wenye nidhamu, kujali na kufuata misingi ya utu, kujitoa kwa jamii katika kutekeleza kanuni na ahadi za Skauti.

Pia Kamishna Mtitu alisema mambo waliojadiliana katika kikao hicho ni muhimu sana katika kuendeleza Skauti na wanakamati wamekubaliana kutekeleza maazimio ya kikao hicho.



Mratibu Mafunzo wa Skauti 
Mkoa wa Dar Es Salaam
Ndugu Mwanyato James
Mwanyato James ambaye ni Mratibu wa Mafunzo Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam alisema katika mahojiano na waandishi wa habari kuwa "Natumai tutayatimiza yote tuliyoyajadili, pia nafuraha sana kuona kikao hiki kimehudhuliwa na watendaji wakuu wote wa Skauti Wilaya za Dar Es Salaam, naomba tuendelee hivi kwa kasi hii kwa maendeleo ya Skauti na jamii yetu"

Kamati imekubaliana kuandaa siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa Skauti Duniani (Founder's Day), Marehemu Paden Pawell aliyezaliwa tarehe 12 Februari 1857 na kufariki tarehe 8 Januari, 1941.

Mwenyekiti Mtitu alitumia fursa katika kikao hicho kuwatambulisha baadhi ya wajumbe wapya ambao ni James Mwanyato (Mafunzo), Mama Ramadevi Sankran Lyer (Kabu), Sameer Somji (Kazi Maalum), Titto Jackson pamoja na Leonard Gerlad Kiloka (Uakilishi wa Vijana) na wengine ni S. Salim (Mambo ya Nje na uhusiano), Reuben Mlay (Vijana), Anthony Meda (Makambi na Mawasiliano) na Bi Annick Verstraelen (Miradi)