Ijumaa, 27 Desemba 2013

MASHINDANO YA SKAUTI AFRIKA MASHARIKI NA KATI


  • Timu ya Tanzania yakabidhiwa bendera kuipeperusha Burundi
Kamishina Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Abdulkarim Shah akiwapa nasaha Timu ya Skauti ya Taifa na baadhi ya Skauti (awapo pichani) kwenda kushiriki mashindano ya Skauti ya Afrika Mashariki na Kati yatakayofanyika nchini Burundi. Kulia ni Naibu Kamishna Mkuu Ndugu Kassim Mchatta na kushoto ni Kamishna Mkuu Msaidizi kitengo cha Jinsia na Mipango ya Vijana (Youth Programme and Gender). Tarehe 26.12.2013 katika kiwanja cha Skauti Makao Makuu Upanga.       

Timu ya Taifa ya Skauti Tanzania imekabidhiwa Bendera ya Taifa na ya Chama cha Skauti Tanzania pamoja na vifaa vyote baada ya kupata mafunzo na mbinu zaidi za Skauti kwenda kushiriki katika mashindano ya Skauti ya Afrika Mashariki na Kati pamoja na kuhudhuria kongamano la Vijana la Skauti nchini Burundi. Timu hiyo inatarajia kuondoka nchini kuelekea Burundi tarehe 29 Desemba 2013 hadi tarehe 04 Januari 2014.

Akikabidhi bendera hizo, Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania Mhe. Shah aliwatakia wawakirishi hao kila la heri na kuwataka Skauti na Watanzania wote kuwaombea mafanikio mema na hatimaye kurudi nyumbani na ushindi. Mheshimiwa Shah alisema, "Ushindi mtakao upata ni wa Tanzania mzima na siyo wa mtu mmoja mmoja, hivyo pamoja na mafunzo na mbinu za Skauti mlizopata, tuna waombea kila lililo la kheri kwa Mwenyezi Mungu mfike salama na mpeperushe vyema bendera ya nchi yetu" aliongeza kwa kusema, "Sisi Skauti na Watanzania wote tupo pamoja nanyi katika safari na katika mashindano hayo, mtuwakirishe vyema"
 
Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania Mheshimiwa Shah akikabidhi bendera ya Skauti Tanzania kwa timu ya Skauti itakayoshiriki mashindano ya Skauti ya Afrika Mashariki na Kati nchini Burundi.

Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania Mheshimiwa Shah akikabidhi bendera ya  Tanzania kwa timu ya Skauti itakayoshiriki mashindano ya Skauti ya Afrika Mashariki na Kati nchini Burundi.
Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania Mheshimiwa Shah (kulia) akiteta jambo na Kaimu Kamishna Mtendaji Ndugu Gerald Mkude (Brigedia Jenerali Mstaafu) katika hafla ya kuwaaga timu ya Skauti ya Taifa katika kiwanja cha Makao Makuu ya Skauti Upanga tarehe 26/12/2013.
Baadhi ya Vijana wa kike wa timu ya Skauti ya Taifa inayokwenda nchini Burundi kwa Mashindano ya Skauti Afrika Mashariki na Kati

Baadhi ya Vijana wa kiume wa timu ya Skauti ya Taifa inayokwenda nchini Burundi kwa Mashindano ya Skauti Afrika Mashariki na Kati

Baadhi ya Vijana wa kiume wa timu ya Skauti ya Taifa inayokwenda nchini Burundi kwa Mashindano ya Skauti Afrika Mashariki na Kati na Kongamano la Vijana la Skauti wakicheza moja ya ngoma ya kimila Tanzania.

Kamishna Mkuu Mheshimiwa Shah (mwenye miwani) katika picha ya pamoja na baadhi ya Skauti na timu ya Skauti ya Taifa inayokwenda nchini Burundi kwa Mashindano ya Skauti Afrika Mashariki na Kati (mtsari mbele wa pili kulia mwenye furana nyeusi ni Naibu Kamishna Mkuu ndugu Kassim Mchatta)
Baadhi ya vijana wa timu ya Skauti ya Taifa wakionyesha jambo katika viwanja vya Makao Makuu ya Skauti Upanga tarehe 26.12.2013

Baadhi ya vijana wa timu ya Skauti ya Taifa wakiteta jambo katika viwanja vya Makao Makuu ya Skauti Upanga tarehe 26.12.2013

Timu ya Skauti ya Taifa itakayoshiriki mashindano ya Skauti nchini Burundi