Alhamisi, 25 Julai 2013

MAKAMISHNA WAKUU WASAIDIZI WAAPISHWA

  • KAMATI YA UENDESHAJI YAKAMILIKA

Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania Mhe. Abdulkarim Esmail Hassan Shah [MB] (kushoto) akimkabidhi waranti Mkufunzi Skauta Stewart Kiluswa baada ya kumwapisha kuwa Kamishna Mkuu Msaidizi kitengo cha Makao Makuu Hati na Usajili wa Chama cha Skauti Tanzania, tarehe 24 Julai, 2013 katika Ukumbi wa Skauti Makao Makuu Upanga, jijini Dar Es Salaam.

Chama cha Skauti Tanzania kinazidi kukamilisha safu ya juu ya uongozi, Kamishna Mkuu Mhe. Shah (MB) tarehe 19 Julai 2013 alimwapisha Naibu Kamishna Mkuu Skauta Rashid Kassim Mchatta. Katika Kamati ya Uendeshaji hii mpya ambayo wapo waliorudi katika kamati na wengine wapya, pia wapo waliokuwa Makamishna wa Wilaya. Kati ya Makamishna Wakuu Wasaidizi kumi na moja wapya, watano walikuwepo katika kamati iliyoisha muda wake na sita ni wapya. 

Kwa mujibu wa Katiba ya Chama cha Skauti Tanzania, ya mwaka 1997 kifungu 6.5 (e) (vi) Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania amewateuwa na kuwaapisha Makamishna Wakuu Wasaidizi wa Chama cha Skauti Tanzania. Makamishna Wakuu Wasaidizi hao 11 ni katika kukamilisha Kamati ya Uendeshaji katika Chama cha Skauti Tanzania, na kushughulikia vitengo vya, Utawala Bora, Makao Makuu Hati na Usajili, Mafunzo na Rasilimali Watu, Maafa, Majanga na Uokoaji, Jinsia na Mipango ya Vijana, Makambi, Miradi na Maendeleo, Program za Skauti wa Kiislam, Program za Skauti wa Kikristo, Utunzaji na Mazingira, Kazi Maalum na Mambo ya Nje, Teknolojia, Habari, Mawasiliano na Jota Joti (International Affairs and Jota Joti).
Askofu Gervas Nyaisonga aliteuliwa kuwa Kamishna Mkuu Msaidizi anayeshughulikia kitengo cha Program za Skauti wa Kikristo, ambaye alikuwepo katika Kamati iliyoisha muda wake na kuteuliwa kuendelea na nafasi hiyo tena, hakuwepo katika uapisho huo kwasababu za kikazi ambapo anategemewa kuapishwa siku zijazo hivi karibuni.


Mkufunzi John Lusunike

 Mkufunzi wa Skauti, Skauta John Lusunike
Kamishna Mkuu Msaidizi atakayeshughulikia Utawala Bora (Good Governance), yeye ni Kamishna Mkuu Msaidizi mpya kushika nafasi hii katika Kamati ya Uendeshaji.








Mkufunzi Omari Mavura
Mkufunzi wa Skauti, Alhaj Omari Mavura alishawai kuwa Kamishna Mkuu Msaidizi anayeshughulikia kitengo cha Mipango ya Vijana (Youth Program), Hati na Usajili (Warrant and Registration), Maafa, Majanga na Uokoaji (Risk Management and Disaster) na Jota/Joti ambaye kwa sasa anashughulikia kitengo cha Program za
Skauti wa Kiislam (Muslim Scouts Program)



Faustin Magige



Skauta Faustin Magige alikuwepo katika Kamati ya Uendeshaji iliyoisha muda wake ambapo alikuwa Naibu Kamishna Mkuu, kwa sasa anashughulikia kitengo cha Kazi Maalum (Special Duty).







Egnetha Manjoli


Skauta  Egnetha Manjoli, ni mmoja kati ya wapya katika Kamati hii na anashughulikia kitengo cha Makambi na Kazi za nje (Campsite and Outreach) 









Fredrick .P. Nguma

Skauta Fredrick Peter Nguma, amerudi tena katika nafasi ya kitengo cha Mambo ya Nje, Teknolojia, Habari, Mawasiliano na Jota Joti (International Affairs). Kitengo hiki kimeunganishwa na kitengo cha zamani cha Mawasiliano na Jota Joti ambacho alikuwa anakishughulikia Skauta Hidan Ricco

 
Juma Massudi

Skauta Juma Massudi alikuwepo katika kamati iliyoisha muda wake akishughulikia kitengo cha Hati na Usajili (Warrant and Registration), kwa sasa anashughulikia kitengo cha Maafa, Majanga na Uokoaji (Risk Management and Disaster)







Mkufunzi Stewart Kiluswa
Mkufunzi wa Skauti, Skauta Stewart Kiluswa ni miongoni ya wapya Makamishna Wakuu Wasaidizi katika Kamati ya Uendeshaji, anashughulikia kitengo cha  Makao Makuu Hati na Usajili (HQ Warrant and Registration)








 
Hamis Kerenge Masasa
 Skauta Hamis Kerenge Masasa kabla ya uteuzi wake huu mpya alikuwa Kamishna wa Skauti wa Mkoa wa Pwani, kwa sasa ni Kamishna Mkuu Msaidizi kitengo cha Miradi na Maendeleo (Project and Development)


Mkufunzi Abdallah Sakasa
Mkufunzi wa Skauti Abdallah Sakasa katika historia ya Chama cha Skauti Tanzania alishawai kuwa Kaimu Kamishna Mkuu na Katibu wa Kamati ya Mpito ambayo iliteuliwa na Rais wa Chama cha Skauti ambaye ni Waziri wa Elimu Dkt. Shukuru Kawambwa. Kwa sasa ameteuliwa kushika nafasi ya Kamishna Mkuu Msaidizi anayeshughulikia kitengo cha Rasilimali Watu na Mafunzo (Adult Resource and Training)



Mkufunzi Mary Anyitike
Mkufunzi Skauta Mary Anyitike ni mmoja wapo waliokuwa katika Kamati iliyoisha muda wake, katika historia ya Chama inaonyesha kuwa alishawai kuwa Kamishna Mkuu Msaidizi kitengo cha Mipango ya Vijana (Youth Program) na kitengo cha Rasilimali Watu na Mafunzo (Adult Resource and Training) na sasa amerudi tena nafasi ya
Jinsia na Mipango ya Vijana (Youth Program and Gender)


Amina Maulidi 
Skauta Amina Maulidi aliyekuwa Kamishna wa Skauti wa Wilaya ya Ilala, ameteuliwa kushika nafasi ya Kamishina Mkuu Msaidizi anayeshughulikia kitengo cha Utunzaji na Mazingira (Environment and Conservation)  






Pamoja na kuwaapisha Makamishna Wakuu Wasaidizi hao, Kamishna Mkuu Mhe. Shah (MB) aliwaasa Skauti wote kufanyakazi kwa weledi na moyo wa kujitolea katika kuleta maendeleo ya Chama, pia kuvunja makundi na kutokuwa na maneno ya pembeni, fitina na hatimaye kukipaka matope Chama cha Skauti Tanzania, Mhe. Shah alisema "Sitokubali kuchafuliwa mimi binafsi, Mlezi wa Chama, Rais wa Chama, Skauti Mkuu, Wadhamini wa Chama, Naibu Kamishna Mkuu, Makamishna Wakuu Wasaidizi, Skauti wenzangu na yeyote atakaye kiuka taratibu za Chama cha Skauti hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake"

Kamishna Mkuu Mhe. Abdulkarim Shah (Mb) (wanne kutoka kushoto) katika picha ya pamoja na Makamishna Wakuu Wasaidizi na baadhi ya viongozi wa Skauti nje ya Makao Makuu ya Chama cha Skauti Upanga jijini Dar Es Salaam tarehe 24 Julai, 2013. Baada ya kuwaapisha Makamishna Wakuu Wasaidizi.

Jumamosi, 20 Julai 2013

KAMISHNA MKUU AFUTA WARANTI ZA MAKAMISHNA SKAUTI WOTE

  • ATOA TAARIFA KWA WANACHAMA WA CHAMA CHA SKAUTI TANZANIA
  • KUFANYIKA KWA KAMBI YA TAIFA YA VETERANI
  
Kamishna Mkuu Mhe. Abdulkarim Shah (Mbunge wa Mafia na Mwenyekiti wa Wabunge Skauti Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akitoa taarifa kwa wanachama wa Skauti Tanzania tarehe 19 Julai, 2013 katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Skauti, Upanga jijini Dar Es Salaam.

Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania (pia Mbunge wa Mafia na Mwenyekiti wa Skauti Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) Mhe. Abdulkarim Esmail Hassan Shah, akizungumza kabla ya kutoa taarifa yake, alizungumzia kero ambazo dhahiri zinaonyesha kutokuwa na heshima, nidhamu na kusahau kanuni na ahadi ya Skauti kwa baadhi ya Skauti wachache. Kamishna Mkuu Mhe. Shah alikumbusha kuwa ni wajibu wa kila Skauti kufuata taratibu, ahadi, kanuni na katiba ya chama cha Skauti.
Kamishna Mkuu alisema, "Kero yangu ipo kwa baadhi ya Skauti kusambaza ujumbe mfupi maandishi wa simu ya kiganjani, wenye maneno yasiyofaa" Mhe. Shah aliendelea kusema, "ndugu zangu Skauti, tusubiri tujichafue wenyewe sio kuanza kutuchafua" Kamishna Mkuu alisisitiza kwamba hatua kali na za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya Skauti yeyote hasiyefuata taratibu za Skauti.

Nae Naibu Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania ndugu Rashid Kassim Mchatta, katika salaamu zake za kushukuru kwa kuteuliwa na kuapishwa kwa nafasi hiyo alisema, "Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa hatua hii, sina mengi ya kusema zaidi ya kuahidi kushirikiana na Skauti wote, lakini siko tayari kushirikiana na Skauti ambaye hataki kutimiza wajibu wake, kufuata kanuni, ahadi na katiba ya chama chetu"

Katika taarifa yake kwa wanachama wa chama cha Skauti Tanzania, Kamishna Mkuu wa Skauti Mhe. Shah alisema;

"1. Kufuatia Mkutano Mkuu Maalum wa Baraza Kuu la Skauti uliofanyika tarehe 05 Januari 2013, majina matatu ya wagombea wa nafasi ya Skauti Mkuu yaliwasilishwa kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mlezi wa Chama cha Skauti Tanzania.
Mgeni wa heshima ambaye ndiye mdhamini wa Chama cha Skauti Tanzania Mzee Ally Hassan Mwinyi (Rais mstaafu) [katikati] akijiandaa kutoa hutuba katika Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu ulifanyika tarehe 05 Januari 2013 katika ukumbi wa Don Bosco Upanga Dar Es Salaam. Kulia ni Rais wa Chama cha Skaut Mh. Shukuru Kawambwa (Waziri wa Elimu) na kushoto ni Prof. W. Salungi (Makamo Mwenyekiti) wa mkutano mkuu.

2. Kwa madaraka aliyonayo katika katiba ya Chama cha Skuti Tanzania, Mlezi wa Chama alimteua na kumuapisha Mheshimiwa Mwantumu Bakari Mahiza kuwa Skauti Mkuu (Chief Scout). Hii ilikuwa tarehe 24 Juni, 2013.
Rais Dkt.Jakaya Kikwete akimuapisha Skauti Mkuu Mhe. Mwantum Mahiza Ikulu Juni 24, 2013
Mhe. Abdulkarim Shah akiapa kuwa Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania, tarehe Julai 12, 2013
3. Baada ya uteuzi wa Skauti Mkuu, Kamati Tendaji ya Chama ilifanya Mkutano Maalum wa uchaguzi wa Kamishna Mkuu (Chief Commissioner) wa Chama. Kwa kuzingatia katiba ya Chama, Kamati iliwasilisha majina ya wagombea kwa Skauti Mkuu kwa ajili ya uteuzi. Skauti Mkuu ameniteua na kuniapisha mimi Abdulkarim Esmail Hassan Shah kuwa Kamishna Mkuu. Hii ilikuwa tarehe 12 Julai, 2013.
Naibu Kamishna Mkuu, Ndugu Mchatta akiapa kushika nyadhifa hiyo

4. Katika hatua ya kuendelea kukamilisha safu ya Uongozi, leo (tarehe 19 julai, 2013) nimemuapisha Ndugu Rashid Kassim Mchatta kuwa Naibu Kamishna Mkuu (Deputy Chief Commissioner) wa Chama cha Skauti Tanzania. Aidha uteuzi wa Makamishna Wakuu Wasaidizi (Assistant Chief Commissioner) utafanyika hivi punde. Hawa kwa pamoja watakamilisha safu ya uongozi katika Kamati ya uendeshaji.
5. Ili kuimarisha uongozi wa Chama Mikoani na Wilayani nitatoa waraka wa kutengua madaraka kwa waliokuwa Makamishna na Manaibu wao Mikoani na Wilayani. Kikatiba nafuta waranti za Makamishna wote na zinatakiwa kurejeshwa Makao Makuu ya Chama ifikapo tarehe 15 Agosti, 2013. Uteuzi wa Makamishna wapya utafanywa katika siku chache zijazo. Katika kipindi hichi cha mpito, Makamishna wa Mikoa na Wilaya wataendesha ofisi hadi hapo uteuzi mpya utakapofanywa.

6. Natoa wito wa ushirikiano kutoka kwa viongozi na wanachama wote ili zoezi hili la kupata safu nyingine ya uongozi likamilike kwa kuzingatia kauli mbiu ya "UONGOZI IMARA CHAMA IMARA"
 
Baadhi ya wanachama wa Chama cha Skauti Tanzania wakimsikiliza Kmishna Mkuu (hayupo katika picha) wakati akitoa taarifa yake kwa wanachama wote wa Skauti Tanzania katika ukumbi wa Makao Makuu ya Chama hicho Upanga jijini Dar Es Salaam tarehe 19 Julai, 2013
Pamoja na taarifa hiyo kwa wanachama wote wa Chama cha Skauti Tanzania, Kamishna Mkuu Mhe Shah alipongeza na kutoa hongera kwa kazi nyingi za kujitolea zilizofanywa na zinazoendelea kufanyika na Skauti Tanzania, vilevile Mhe. Shah aligusia kufanyika kwa kambi ya Taifa ya Skauti wa zamani (Veterani) kuanzia tarehe 16 hadi 18 Agosti, 2013.

Kamishna Mkuu wa Skauti alimpa majukumu ya uandaaji wa kambi hiyo na kumwagiza Kaimu Kamishna wa Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam ndugu Abubakar Mtitu, kuunda kikosi kazi (Task Force) cha kushirikiana kukamilisha kambi hiyo, kwa kufuata na kuzingatia taratibu na maamuzi ya vikao kabla ya kambi hiyo.

Tufuate Twitter: @DarScout http://www.twitter.com/DarScout

Ijumaa, 19 Julai 2013

SAFU YA UONGOZI SKAUTI YAZIDI KUKAMILIKA

  • NAIBU KAMISHNA MKUU AAPISHWA
Chama cha Skauti Tanzania chazidi kukamilisha safu ya viongozi wake wa juu.
Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mlezi wa Skauti Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kumteuwa na kumuapisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani ambaye ni Skauti Mkuu Mhe. Mwantumu Mahiza, nawe Skauti Mkuu alimuapishwa Kamishna Mkuu kwa kufuata katiba na kanuni za Skauti.
Kamishna Mkuu Mhe. Abdulkaim Shah pia ni Mbuge wa Mafia (kushoto) akimwapisha Naibu Kamishna Mkuu Rashid Mchatta (katikati) tarehe Julai 19, 2013 katika ukumbi wa makao makuu ya Skauti Upanga, jijini Dar Es Salaam.
Katika hali ya kutaka kuhakikisha chama kinakuwa na mwelekeo mzuri na kurudisha heshima kwa kufuata kanuni na katiba ya Skauti, Kamishna Mkuu amemteua na kumuapisha Naibu Kamishna Mkuu Rashid Kassim Mchatta, tarehe Julai 19, 2013 katika ofisi za Makao Makuu ya Skauti Tanzania Upanga, jijini Dar Es Salaam.
Kamishna Mkuu Mhe. Abdulkaim Shah pia ni Mbuge wa Mafia akisaini Kiruhusishi (Warrant) ya Naibu Kamishna Mkuu baada ya kumuapisha tarehe Julai 19, 2013 katika ukumbi wa makao makuu ya Skauti Upanga, jijini Dar Es Salaam.
Kamishna Mkuu Mhe. Abdulkaim Shah pia ni Mbuge wa Mafia (kushoto) akimkabidhi kiruhusishi (Warrant) Naibu Kamishna Mkuu Rashid Mchatta (kulia) tarehe Julai 19, 2013 katika ukumbi wa makao makuu ya Skauti Upanga, jijini Dar Es Salaam.
Kiruhusishi (Warrant) cha Naibu Kamishna Mkuu Rashid Mchatta
Picha ya pamoja Kamishina Mkuu pamoja na baadhi ya viongozi wa Skauti waliohudhuria kuapishwa kwa Naibu Kamishna Mkuu.

Alhamisi, 18 Julai 2013

Dar Es Salaam Local Scouts Association: TANZIA...TANZIA...

Dar Es Salaam Local Scouts Association: TANZIA...TANZIA...: Chama cha Skauti Tanzania kipo katika majonzi makubwa baada ya kufikwa na msiba wa Skauti pamoja na kufiwa kwa wazazi wa baadhi ya Skauti....

TANZIA...TANZIA...

Chama cha Skauti Tanzania kipo katika majonzi makubwa baada ya kufikwa na msiba wa Skauti pamoja na kufiwa kwa wazazi wa baadhi ya Skauti.
Marehemu Skauta Frank Msina amefariki dunia tarehe Julai 16, 2013.
Marehemu Skauta Frank Msina enzi za uhai wake

Marehemu Frank Msina wakati wa uhai wake aliwahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi katika Chama cha Skauti Tanzania.

Wasifu wa marehemu kwa mujibu wa mahojiano kwa njia ya simu na mkufunzi wa Skauti, Skauta Stewart Kiluswa alisema, "marehemu Msina mwaka 1977 alikuwa Skauti katika kundi la Shule ya Sekondari ya Shabani Robert jijini Dar Es Salaam, kati ya mwaka 1978 na 1979 alikuwa kiongozi msaidizi wa kundi la Shule ya Msingi Makulumla  na Karume jijini Dar Es Salaam, mwaka 1998 mpaka 2000 alikuwa Naibu Kamishna wa Skauti wa Mkoa wa Dar Es Salaam, 2000 mpaka 2001 alishika nafasi ya uongozi ya Kamishna wa Mkoa wa Dar Es Salaam. Mwaka 2001 hadi 2010 aliishi nchini Uingereza. Marehemu Msina alikuwa miongoni mwa wanachama wa Skauti Tanzania waliogombea nafasi ya Kamishna Mkuu mnamo tarehe Julai 06, 2013"

Msiba upo nyumbani kwa marehemu Gongo la Mboto, Kipunguni. Marehemu Frank Msina atazikwa tarehe Julai 20, 2013 katika makaburi ya Buguruni Malapa  saa saba mchana.

Pamoja na msiba huo, baadhi ya skauti waliofikwa na msiba ni Skauta Osimundi Kipengele, ambaye amefiwa na baba yake mzazi Mzee Andrea Mchumo Kipengele. Marehemu Mzee Kipengele amefikwa na mauti alfajiri ya tarehe Julai 18, 2013 nyumbani baada ya kulazwa na kuruhusiwa kutoka katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipolazwa. Msiba upo nyumbani kwa Osimundi Kipengele Yombo Machimbo, mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa Mkoani Lindi tarehe Julai 19, 2013 na mazishi yatafanyika Kilwa Kipatimo siku ya Jumamosi tarehe Julai 20, 2013 katika hosipitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa.

Msiba mwingine ni wa baba wa mlinzi wa makao makuu ya Skauti ndugu Ally Masisi ambaye amefiwa na baba yake mzazi Mzee Masisi.
Marehemu Mzee Masisi amefikwa na mauti tarehe Julai 17, 2013 katika hosipitali ya Taifa ya Muhumbili mjini Dar Es Salaam. Msiba upo nyumbani kwa marehemu Mbagala. Mazishi yatafanyika Mkamba, Kisarawe tarehe Julai 18, 2013.

Skauti wote tunaombwa kuhudhuria na kutoa rambirambi zetu kwa wafiwa.

Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi...AMINA.

Ijumaa, 12 Julai 2013

KAMISHNA MKUU AAPISHWA

  • Safu ya Uongozi ya Skauti yaanza kukamilika
    • Gerald Mkude ateuliwa kukaimu Kamishna Mtendaji 
Chama cha Skauti Tanzania kimeweka historia nyingine baada ya kuapishwa kwa Kamishna Mkuu mpya kwa mwaka 2013 - 2016.
Skauti Mkuu Mhe. Mwantum Mahiza (Mkuu wa Mkoa wa Pwani) akimwapisha Kamishna Mkuu (hayupo katika picha) tarehe Julai 12, 2013 katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, mjini Kibaha.


Mhe. Abdulkarim Shah (Mbunge wa Mafia na Mwenyekiti wa  Kikundi cha Skauti wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) akiapa kuwa Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania, tarehe Julai 12, 2013 katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, mjini Kibaha.
Skauti Mkuu Mhe. Mahiza akisaini Kiruhusishi (Warrant) baada ya kumuapisha Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania, tarehe Julai 12, 2013 katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, mjini Kibaha.

Skauti Mkuu Mhe. Mwantum Mahiza (kulia) akisalimiana na Kamishna Mkuu Mhe. Shah baada ya kuapishwa kuwa Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania, tarehe Julai 12, 2013 katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, mjini Kibaha.

Skauti Mkuu Mhe. Mwantumu Mahiza (Mkuu wa Mkoa wa Pwani) amemuapisha Mhe. AbdulKarim Shah (Mbunge wa Mafia na Mwenyekiti wa Kikundi cha Skauti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) kuwa Kamishna Mkuu. Mhe. Shah aliongoza kwa kura nyingi katika uchaguzi uliofanyika siku ya Jumamosi tarehe 06 Julai, 2013 katika ukumbi wa makao makuu ya Skauti jijini Dar es Salaam.

Katika uchaguzi huo ambao ulikuwa na wagombea wapatao 9. Idadi ya Kura na majina ya wagombea hao ni Mhe. AbdulKarim Shah (24), Faustin Magige, Rashidi Mchata (19), Hamisi Masasa (11), Mathusela Magoti (3) wengine ni Pharas Magesa (19), Osmundi Kipengele (4), Lawrence Muhomwa (8) na Frank Msina (5).

Kuelekea katika uchaguzi huo, Kamishna Faustin Magige alijiengua katika kinyang'anyiro hicho na kufanya kubakia wagombea 8.
 
Mhe. Shah alipata idadi ya kura nyingi, akifuatiwana Rashidi Mchata na Pharas Magesa kwa kufungana kwa kura. 

Skauti Mkuu Mhe. Mwantum Mahiza (kushoto) katika picha ya pamoja na Kamishna Mkuu Mhe. Shah baada ya kuapishwa Kamishna Mkuu tarehe Julai 12, 2013 katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, mjini Kibaha.

Skauti Mkuu Mhe. Mwantum Mahiza (katikati) katika picha ya pamoja na Kamishna Mkuu Mhe. Shah (kushoto) na kulia ni Gerald Mkude (Kaimu Kamishna Mtendaji) baada ya kuapishwa Kamishna Mkuu tarehe Julai 12, 2013 katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, mjini Kibaha.

Kamishna Mkuu Mhe. Shah (kulia) katika picha ya pamoja na ndugu James .J. Warburg Katibu wa Kikundi cha wabunge Skauti wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya shughuli za Bunge - Bunge la Tanzania, tarehe Julai 12, 2013 katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, mjini Kibaha.
 Katika hotuba fupi baada ya kumuapisha Kamishna Mkuu, Skauti Mkuu Mhe Mwantumu Mahiza alisema "hatua ya pili ya mchakato wa uongozi wa Skauti Tanzania umekamilika leo" 
Katika hotuba hiyo Skauti Mkuu alisisitiza kuwa Chama cha Skauti ni cha kujitolea na si cha mtu binafsi au kikundi cha watu fulani, uongozi huu kwa kushirikiana na kamati tendaji kuna kazi kubwa ya kuimarisha chama, kurejesha imani na marafiki na kukijengea chama heshima inayostahili, Skauti Mkuu aliendelea kusema, "Katika kufanya hivyo na kufikia malengo, kuna watu ambao watakaoachwa katika madaraka yao waliokuwa nayo sasa ama kuachia wenyewe na kubakia kuwa wanachama wa kawaida wa chama cha Skauti Tanzania"

Pia Skauti Mkuu Mhe. Mahiza alisisitiza Skauti kuzingatia weledi na heshima na kuondoa umimi katika chama. Alitumia nafasi hiyo pia kuwaomba radhi kwa wale watakao guswa na kuachwa katika nafasi mbalimbali za uongozi wa chama na kuacha chama kiendelee. Mwisho Mhe. Mahiza alisema "Simchukii mtu naomba tupishane ili kujenga chama cha Skauti"

Skauti Mkuu Mhe. Mahiza, alimteua Gerald Mkude (aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya mpito) kuwa Kaimu Kamishna Mtendaji mpaka hapo  atakapopatikana kamishna mtendaji wa kuajiriwa.
Kamishina wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Abubakar Mtitu (kushoto) na Juma Massudi (Kulia) ni baadhi ya Viongozi waliohudhulia kuapishwa kwa Kamishna Mkuu tarehe Julai 12, 2013 katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, mjini Kibaha.

Hamisi Masasa Kamishna wa Mkoa wa Pwani (kushoto) na Faustin Magige (kulia) baadhi ya Viongozi waliohudhulia kuapishwa kwa Kamishna Mkuu tarehe Julai 12, 2013 katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, mjini Kibaha.
Katika salamu zake za kushukuru Mhe. Shah alisisitiza kuwa na umoja, kuondoa makundi na kuweka mshikamano kwa maendeleo ya wote huku akisisitiza kufuata katiba, kanuni na ahadi ya chama cha Skauti Tanzania.

"Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuwepo na kupata nafasi hii katika chama cha Skauti Tanzania, nitafuata katiba, kanuni na ahadi ya Skauti katika kutekeleza majukumu yangu haya" alisema Mhe. Shah.

Pia alisisitiza kuheshimu kila mtu bila ya kuangalia umri, kulinda heshima kwa kila mmoja pamoja na kushirikiana na kamati tendaji, Skauti na viongozi wengine kwa busara na kufanyakazi kwa uwezo wake katika kuleta na kusimamia mabadiliko ya maendeleo katika chama.
Viongozi waliohudhulia kuapishwa kwa Kamishna Mkuu tarehe Julai 12, 2013 katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, mjini Kibaha.
Skauti Mkuu Mhe. Mahiza (wa tano kutoka kulia), mwenyekiti wa kamati tendaji Balozi Kuhanga (wa nne kutoka kushoto), Kamishna Mkuu Mhe. Shah (kulia mwa Skauti Mkuu) katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa kamati tendaji na viongozi wengine wa Skauti, tarehe Julai 12, 2013 katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, mjini Kibaha.

SKAUTI MKUU APOKEA ZAWADI

Katika hali iliyomshangaza Skauti Mkuu Mhe. Mwantum Mahiza ni zawadi alizopokea kutoka kwa Kamishna wa Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam Abubakar Mtitu kwa niaba ya Skauti Tanzania. Zawadi hizo ni picha kubwa ya taswira yake iliyochorwa na kinyago cha twiga, wakimtakia utendaji mzuri wa uongozi wake ikiwakama ishara ya wasifu wa mnyama huyo.
Skauti Mkuu Mhe. Mwantum Mahiza (kushoto) akionyesha zawadi mojawapo waliyopewa pembeni yake ni Kamishna Mkuu Mhe. Shah. Tarehe 12 Julai, 2013 katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, mjini Kibaha.
Kamishna wa Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam Abubakar Mtitu akimkabidhi moja ya zawadi Skauti Mkuu Mhe. Mwantum Mahiza. Tarehe 12 Julai, 2013 katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, mjini Kibaha.