Alhamisi, 25 Julai 2013

MAKAMISHNA WAKUU WASAIDIZI WAAPISHWA

  • KAMATI YA UENDESHAJI YAKAMILIKA

Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania Mhe. Abdulkarim Esmail Hassan Shah [MB] (kushoto) akimkabidhi waranti Mkufunzi Skauta Stewart Kiluswa baada ya kumwapisha kuwa Kamishna Mkuu Msaidizi kitengo cha Makao Makuu Hati na Usajili wa Chama cha Skauti Tanzania, tarehe 24 Julai, 2013 katika Ukumbi wa Skauti Makao Makuu Upanga, jijini Dar Es Salaam.

Chama cha Skauti Tanzania kinazidi kukamilisha safu ya juu ya uongozi, Kamishna Mkuu Mhe. Shah (MB) tarehe 19 Julai 2013 alimwapisha Naibu Kamishna Mkuu Skauta Rashid Kassim Mchatta. Katika Kamati ya Uendeshaji hii mpya ambayo wapo waliorudi katika kamati na wengine wapya, pia wapo waliokuwa Makamishna wa Wilaya. Kati ya Makamishna Wakuu Wasaidizi kumi na moja wapya, watano walikuwepo katika kamati iliyoisha muda wake na sita ni wapya. 

Kwa mujibu wa Katiba ya Chama cha Skauti Tanzania, ya mwaka 1997 kifungu 6.5 (e) (vi) Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania amewateuwa na kuwaapisha Makamishna Wakuu Wasaidizi wa Chama cha Skauti Tanzania. Makamishna Wakuu Wasaidizi hao 11 ni katika kukamilisha Kamati ya Uendeshaji katika Chama cha Skauti Tanzania, na kushughulikia vitengo vya, Utawala Bora, Makao Makuu Hati na Usajili, Mafunzo na Rasilimali Watu, Maafa, Majanga na Uokoaji, Jinsia na Mipango ya Vijana, Makambi, Miradi na Maendeleo, Program za Skauti wa Kiislam, Program za Skauti wa Kikristo, Utunzaji na Mazingira, Kazi Maalum na Mambo ya Nje, Teknolojia, Habari, Mawasiliano na Jota Joti (International Affairs and Jota Joti).
Askofu Gervas Nyaisonga aliteuliwa kuwa Kamishna Mkuu Msaidizi anayeshughulikia kitengo cha Program za Skauti wa Kikristo, ambaye alikuwepo katika Kamati iliyoisha muda wake na kuteuliwa kuendelea na nafasi hiyo tena, hakuwepo katika uapisho huo kwasababu za kikazi ambapo anategemewa kuapishwa siku zijazo hivi karibuni.


Mkufunzi John Lusunike

 Mkufunzi wa Skauti, Skauta John Lusunike
Kamishna Mkuu Msaidizi atakayeshughulikia Utawala Bora (Good Governance), yeye ni Kamishna Mkuu Msaidizi mpya kushika nafasi hii katika Kamati ya Uendeshaji.








Mkufunzi Omari Mavura
Mkufunzi wa Skauti, Alhaj Omari Mavura alishawai kuwa Kamishna Mkuu Msaidizi anayeshughulikia kitengo cha Mipango ya Vijana (Youth Program), Hati na Usajili (Warrant and Registration), Maafa, Majanga na Uokoaji (Risk Management and Disaster) na Jota/Joti ambaye kwa sasa anashughulikia kitengo cha Program za
Skauti wa Kiislam (Muslim Scouts Program)



Faustin Magige



Skauta Faustin Magige alikuwepo katika Kamati ya Uendeshaji iliyoisha muda wake ambapo alikuwa Naibu Kamishna Mkuu, kwa sasa anashughulikia kitengo cha Kazi Maalum (Special Duty).







Egnetha Manjoli


Skauta  Egnetha Manjoli, ni mmoja kati ya wapya katika Kamati hii na anashughulikia kitengo cha Makambi na Kazi za nje (Campsite and Outreach) 









Fredrick .P. Nguma

Skauta Fredrick Peter Nguma, amerudi tena katika nafasi ya kitengo cha Mambo ya Nje, Teknolojia, Habari, Mawasiliano na Jota Joti (International Affairs). Kitengo hiki kimeunganishwa na kitengo cha zamani cha Mawasiliano na Jota Joti ambacho alikuwa anakishughulikia Skauta Hidan Ricco

 
Juma Massudi

Skauta Juma Massudi alikuwepo katika kamati iliyoisha muda wake akishughulikia kitengo cha Hati na Usajili (Warrant and Registration), kwa sasa anashughulikia kitengo cha Maafa, Majanga na Uokoaji (Risk Management and Disaster)







Mkufunzi Stewart Kiluswa
Mkufunzi wa Skauti, Skauta Stewart Kiluswa ni miongoni ya wapya Makamishna Wakuu Wasaidizi katika Kamati ya Uendeshaji, anashughulikia kitengo cha  Makao Makuu Hati na Usajili (HQ Warrant and Registration)








 
Hamis Kerenge Masasa
 Skauta Hamis Kerenge Masasa kabla ya uteuzi wake huu mpya alikuwa Kamishna wa Skauti wa Mkoa wa Pwani, kwa sasa ni Kamishna Mkuu Msaidizi kitengo cha Miradi na Maendeleo (Project and Development)


Mkufunzi Abdallah Sakasa
Mkufunzi wa Skauti Abdallah Sakasa katika historia ya Chama cha Skauti Tanzania alishawai kuwa Kaimu Kamishna Mkuu na Katibu wa Kamati ya Mpito ambayo iliteuliwa na Rais wa Chama cha Skauti ambaye ni Waziri wa Elimu Dkt. Shukuru Kawambwa. Kwa sasa ameteuliwa kushika nafasi ya Kamishna Mkuu Msaidizi anayeshughulikia kitengo cha Rasilimali Watu na Mafunzo (Adult Resource and Training)



Mkufunzi Mary Anyitike
Mkufunzi Skauta Mary Anyitike ni mmoja wapo waliokuwa katika Kamati iliyoisha muda wake, katika historia ya Chama inaonyesha kuwa alishawai kuwa Kamishna Mkuu Msaidizi kitengo cha Mipango ya Vijana (Youth Program) na kitengo cha Rasilimali Watu na Mafunzo (Adult Resource and Training) na sasa amerudi tena nafasi ya
Jinsia na Mipango ya Vijana (Youth Program and Gender)


Amina Maulidi 
Skauta Amina Maulidi aliyekuwa Kamishna wa Skauti wa Wilaya ya Ilala, ameteuliwa kushika nafasi ya Kamishina Mkuu Msaidizi anayeshughulikia kitengo cha Utunzaji na Mazingira (Environment and Conservation)  






Pamoja na kuwaapisha Makamishna Wakuu Wasaidizi hao, Kamishna Mkuu Mhe. Shah (MB) aliwaasa Skauti wote kufanyakazi kwa weledi na moyo wa kujitolea katika kuleta maendeleo ya Chama, pia kuvunja makundi na kutokuwa na maneno ya pembeni, fitina na hatimaye kukipaka matope Chama cha Skauti Tanzania, Mhe. Shah alisema "Sitokubali kuchafuliwa mimi binafsi, Mlezi wa Chama, Rais wa Chama, Skauti Mkuu, Wadhamini wa Chama, Naibu Kamishna Mkuu, Makamishna Wakuu Wasaidizi, Skauti wenzangu na yeyote atakaye kiuka taratibu za Chama cha Skauti hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake"

Kamishna Mkuu Mhe. Abdulkarim Shah (Mb) (wanne kutoka kushoto) katika picha ya pamoja na Makamishna Wakuu Wasaidizi na baadhi ya viongozi wa Skauti nje ya Makao Makuu ya Chama cha Skauti Upanga jijini Dar Es Salaam tarehe 24 Julai, 2013. Baada ya kuwaapisha Makamishna Wakuu Wasaidizi.