Jumanne, 10 Februari 2015

SHEREHE ZA KUMBUKUMBU YA MWANZILISHI WA SKAUTI 2015

  • MAANDALIZI YAKAMILIKA KWA ASILIMIA 90
  • JK KUWA MGENI RASMI
 
Chama cha Skauti Tanzania kupitia Kamishina Mtendaji Bi. Eline Kitaly katika taarifa yake kwa njia ya barua pepe kwa Kamishina wa Skauti wa mkoa wa Dar Es Salaam na Kamishina wa Wilaya pamoja na wasaidizi wao (nakala ya barua pepe hiyo DarScout Habari inayo) imesema kuwa maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa na kuwataka kuhamasisha Skauti wao kuhudhuria kwa wingi pamoja na kulipia ada ya uanachama na kukamilisha taratibu zote za "Smart Card".
 


Maandalizi ya Kumbukumbu ya Mwanzilishi wa Skauti Duniani kwa mwaka 2015 yameandaliwa na Makao Makuu kwa kushirikiana na Skauti Mkoa wa Dar es Salaam, yatakuwa ya aina tofauti na ya kipekee zaidi. Wakizungumza na chombo hiki cha habari cha Dar Scout Habari kwa nyakati tofauti, Kamishna wa Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam, Skauta Abubakari Mtitu alisema, "Tumekwisha kamilisha jukumu letu na matayarisho yanaenda vizuri zaidi"
 
Abubakari Mtitu
Kamishna wa Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam

Naye Kamishna Mkuu Msaidizi wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kimataifa, Habari na JotaJoti, Skauta Fredrick Nguma alibainisha kwa kusema, "Mwaka huu katika maazimisho ya kumbukumbu za mwanzilishi wa Skauti duniani, mgeni rasmi atakuwa Mlezi wa chama chetu ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Prof. Jakaya Mrisho kikwete, na maazimisho hayo yatafanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar Es Salaam"


Fredrick Peter Nguma
Kamishna Mkuu Msaidizi wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa kimataifa, Habari na JotaJoti
 

"Katika kuelekea kuazimisha kumbukumbu hiyo, Wito unatolewa kufanya kazi za huduma kwa jamii kwa kujitolea kama ilivyo ada na wajibu wa Skauti" ulisema mtandao USIO RASMI wa WhatsApp wa "Scout Chat - SC". Mtandao huo ulisisitiza kuwa Skauti ni watu wenye nidhamu, kujali na kufuata misingi ya utu, kujitoa kwa jamii katika kutekeleza kanuni na ahadi za Skauti.

Pia majadiliano katika mtandao ambao unazidi kuwa maarufu katika chama na February 02, 2015 umetimiza mwaka mmoja toka uanzishwe, ulisisitiza kuwa mambo wanayoyajadili viongozi katika kikao cha maandalizi ni muhimu sana katika kuendeleza Skauti na wajumbe wa "Scout Chat" wamekubaliana kutekeleza maazimio ya kamati hiyo ya maandalizi.

 

 
 
 Jiunge na Dar Scout Habari:  Scout Chat (SC) WhatsApp +255-655-095559