Jumapili, 13 Januari 2013

Mafunzo ya Kielimu na Ujasiri


Baadhi ya Skauti wakisikiliza maelekezo toka kwa mmoja wa afisa wa ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Arusha (AICC)
Ni desturi ama kawaida ya Skauti ulimwenguni kufanya ziara za mafunzo kwa ajili ya elimu na kuwajengea ujasiri, mafunzo hayo ufanywa kwa kutembelea sehemu mbalimbali za kihistoria, jiografia, kisayansi na mengineyo. Mwezi wa Desemba 2012, Skauti mkoa wa Dar Es Salaam walifanya mafuanzo hayo kwa kufanya utalii wa ndani, kujifundisha jiografia, historia na mengineyo kwa kutembelea eneo la hifadhi ya Ngorongoro, ukumbi wa mikutano ya kimataifa wa Arusha (AICC).
Pamoja na kutembelea hifadhi ya taifa, waliweza kujifunza maisha ya nyoka, wanavyoishi na kuzaliana, kuona na kujifunza maisha ya wanyama, ndege na wadudu. Kujifunza mila na desturi za kabila la Wamasaai, na jinsi gani wanavyoweza kuishi katika hifadhi ya wanyama bila madhara yoyote na kuendeleza kutunza mazingira.

Baadhi ya Skauti wakiwa wamevaa nguo za Kimasaai
Kamishina wa Skauti wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Abubakari Mtitu (aliye vaa furana) akiwa na baadhi ya Skauti waliovaa vazi la Kimasaai katika mafunzo ya kielimu Ngorongoro  Desemba 2012
Skauti wakiwa wamepanda Ngamia Mkoani Arusha katika ziara ya Kielimu na Ujasiri katika Hifadhi ya Taifa ya wanyama Ngorongoro.
Skauti wakiangalia bonde la hifadhi ya Ngorongoro

Ziara nyingine ilikuwa Hong Kong, uko Skauti waliweza kutembelea chuo cha mafunzo cha Skauti wa majini (Pak Sha Wan " Sea activity training block) wa mji wa Hong Kong nchini China  pamoja na "DREAM ISLAND".

Baadhi ya Skauti wa Mkoa wa Dar Es Salaam wakiwa katika chuo cha mafunzo cha Skauti wa majini Hong Kong Desemba 2012 wakipata maelekezo.
Skauti wakiwa wanaangalia mandhali karibu na chuo cha Skauti wa majini (baharini) Hong Kong walipokwenda katika ziara ya mafunzo ya Kielimu na Ujasiri, wa mbele kushoto alivaa sare ni Juma Massudi kulia ni Skauti wa Hong Kong mwenyeji wao na nyuma aliyevaa shati jeupe na mistari ya viboksi ni Faustin Magige viongozi wa ziara hiyo, Desemba 2012.



Jumapili, 6 Januari 2013

Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la Skauti la Warejesha Mwenyekiti na Katibu

Mgeni wa heshima ambaye ndiye mdhamini wa Chama cha Skauti Tanzania Mzee Ally Hassan Mwinyi (Rais mstaafu) [katikati] akijiandaa kutoa hutuba katika Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu ulifanyika tarehe 05 Januari 2013 katika ukumbi wa Don Bosco Upanga Dar Es Salaam. Kulia ni Rais wa Chama cha Skaut Mh. Shukuru Kawambwa (Waziri wa Elimu) na kushoto ni Prof. W. Salungi (Makamo Mwenyekiti) wa mkutano mkuu.

Mkutano Kuu wa Baraza Kuu la Skauti Tanzania uliofanyika tarehe 05 Januari 2013 katika Ukumbi wa Don Bosco uliopo Upanga jijini Dar Es Salaam umewarejesha madarakani tena Mwenyekiti na Katibu wa Kamati Tendaji iliyopita.

Mkutano mkuu huo, ulioandaliwa na Kamati ya mpito ya Skauti chini ya mwenyekiti wake Brigedia Jenerali mstaafu G. Mkude. Kamati hiyo ya mpito ilichaguliwa baada ya Rais wa Chama cha Skauti Tanzania kuwaachisha madaraka Viongozi waliokuwa madarakani kwa muda wao kuisha.

Mkutano mkuu uliongozwa na mwenyekiti wa mkutano ambaye ni Rais wa Chama cha Skauti Waziri wa Elimu (kwa mujibu wa Katiba ya Skauti) Mhe. Shukuru Kawambwa, ulifunguliwa na mgeni rasmi ambaye ni mdhamini wa chama cha Skauti Mhe. Ally Hassani Mwinyi (Rais Mstaafu)Kabla ya kuanza kwa Mkutano mkuu, uhakiki wa wajumbe ulianza saa 1:00 asubuhi Makao Makuu ya Skauti Upanga.
Wagombea wa nafasi ya Skauti Mkuu wakifuatilia kwa makini Uchaguzi huo, Mhe. Mwantumu Mahiza - Mkuu wa Mkoa wa Pwani (kushoto) na Mhe. Abdulkarim Shah - Mbunge wa Mafia (Kulia aliyevaa miwani)

WALIO GOMBEA

Mkutano mkuu wa Baraza kuu ulikuwa na ajenda moja muhimu ambayo ni uchaguzi wa majina matatu ya Skauti Mkuu, Mwenyekiti, Makamo Mwenyekiti na Katibu wa kamati tendaji pamoja na wajumbe wake wanane.


Wanachama wa chama hicho waliojitokeza kugombea nafasi ya Skauti Mkuu walikuwa ni watano ambao ni; Mh. Mwantumu .B. Mahiza (Mkuu wa Mkoa wa Pwani), Aron Titus Kagurumjuli, Iddi Omari Kipingu (Kanali Mstaafu), Mh. Abdulkarim .E. .H. Shah (Mbunge wa Mafia, Mwenyekiti wa kamati ya Skauti Wabunge na kamati ya Bunge ya Ardhi na Mazingira) na Mika Elia Mlonganile (Mwenyekiti wa Skauti wa halmashauri ya Njombe).
Mh. Mwantumu Mahiza
Mh. AbdulKarim Shah





















Kwa upande wa nafasi ya Mwenyekiti wa kamati tendaji, pia ilikuwa na idadi ya watu watano: Alfred Mwambeleko, Gosbert Njunwa, Mh. Mohamed Abdulaziz, Balozi Nicolaus .A. Kuhanga na Zulu Ally Lyana.


Balozi Nicolaus Kuhanga
Mh. Mohamed Abdulaziz






















Nafasi ya makamo wa Mwenyekiti wa kamati tendaji; Nuru Hepautwa, Mwaking'inda na Katabalo.


Nafasi ya Katibu wa kamati tendaji; Angelius Liganga, Henrick Bambo, J. Kanumba, Khamis .S. Khamis na Mwanaamina Kombakono.

Katika nafasi ya Wajumbe wa kamati tendaji ilikuwa na wagombea kumi na saba na waliotakiwa ni wajumbe nane tu, waliogombea nafasi hiyo ni: Annie Faith Kibira, Cleophace Rutta, Deogratias Lubuva, Fatma Salum Abdallah, Fatuma .A. Kange, Fredrick .J. Kaspan, Imam .H. Daffa, Khalid Gachau Mwinshehe, Magdalena .M. Lyaruu, Maulid .B. Kitenge, Merchades .K. Oswald, Michael .N. Meli, Peter Simon Bhokhe, Ramadhan Juma Selungwi, Salehe Ramadhan Msabaha, Tabia Massudi na Victus .S. Stambuli.

Baadhi ya Wajumbe wakisiliza jambo katika
 Mkutano wa Baraza Kuu
Uchaguzi Ulivyoendeshwa; Zoezi zima la uchaguzi lilikuwa la haki na demokrasia. Wajumbe waliohudhuria walitumia nafasi yao kwa haki kikatiba, zoezi lote lilitawaliwa na utulivu pamoja na amani japokuwa palikuwa na vuta nikuvute ya hapa na pale kabla ya kuanza uchaguzi, pamoja na yote kubwa kufuatwa kwa Katiba kulipelekea kumalizika kidemokrasia.



Maoni; "Kwa uchache katiba ya Skauti Tanzania haijajitoshereza ina mapungufu, ni heri ile ya zamani iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2011 kule Bagamoyo na Chama hakina Kanuni, kwahiyo kuna haja ya kutungwa kwa kanuni" alisema Boniface Donnis Mjumbe toka mkoani Mbeya.

"Matokeo mazuri, kidemokrasia wajumbe waliofika wamepata haki zao kikatiba ya chama cha Skauti Tanzania" alisema Fredrick Peter Nguma.


MATOKEO YA UCHAGUZI


Matokeo ya uchaguzi ulioendeshwa kwa haki na usawa (Demokrasia) yalizidisha furaha kwa kila mjumbe aliyehudhulia, hakika mkulima upanda alichovuna!!


SKAUTI MKUU.


Kwa mujibu wa katiba ya Chama cha Skauti Tanzania, Wajumbe wa Mkutano mkuu wa baraza kuu wao uchagua majina matatu ambayo Rais wa chama hicho (Waziri wa Elimu) uyapeleka kwa mlezi wa chama ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiye mwenye mamlaka ya kupitisha/kuteuwa jina moja tu ambaye ndiyo Skauti Mkuu. Wajumbe walioudhulia walikuwa ni 120 walitumia haki yao kikatiba kwa kuwapigia kura wagombea wa nafasi hiyo na matokeo ya maamuzi ya wajumbe yalikuwa hivi [IDADI YA KURA KATIKA MABANO]; 

Mh. MWANTUMU .B. MAHIZA (47), Mh. ABDULKARIM SHAH (22), ARON TITUS KAGURUMJULI (22), IDDI OMARI KIPINGU [Kanali Mstaafu] (17) na MIKA ELIA MLONGANILE (10), idadi ya kura 2 ziliharibika na kuwa jumla ya kura 120 zilizopigwa.
Mh. Mwantumu Mahiza akipongezwa kwa kucheza na Iddi Omari Kipingu kwa kuibuka na kura 47, katika uchaguzi wa Skauti Mkuu, Kipingu akupata kura stahili. "Asiye kubali kushindwa si mshindani" 
Kwa matokeo hayo, bila hajizi wala kupepesa macho! majina matatu yatakayopelekwa kwa Mlezi wa Chama cha Skauti Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania) ni Mh. Mwantumu Mahiza, Mh. Abdulkarim Shah na Aron Titus Kagurumjuli. Subira zaidi inahitajika kwa kipindi hiki ambacho anasubiriwa Mlezi wa Chama kumpitisha mmoja wao kuwa SKAUTI MKUU.


MWENYEKITI KAMATI TENDAJI


Mwenyekiti Balozi Nicolaus Kuhanga kulia
akiwa na Katibu Bi. wanaamina Kombakono 
wajumbe waliendelea kumpadhamana Mwenyekiti wa zamani ambaye alitetea nafasi hiyo. Matokeo yalikuwa hivi [IDADI YA KURA KATIKA MABANO]; 


Balozi Nicolaus .A. Kuhanga (43), Gosbert Njunwa (31), Mh. Mohamed Abdulaziz (23), Alfred Mwambeleko (10) na Zulu Ally Lyana (10) pamoja na matokeo hayo kura 2 ziliharibika.


Kwa matokeo hayo, mwenyekiti wa Mkutano alimtangaza balozi Nicolaus .A. kuhanga kuwa mshindi wa uchaguzi kwa nafasi hiyo.

MAKAMO MWENYEKITI KAMATI TENDAJI

Kwa upande wa makamo mwenyekiti kamati tendaji Ndugu Mwaking'inda alijizolea kura 69, Nuru hepautwa kura 32, Ndugu Katabalo kura 14 na kura zilizohalibika ni 2.

Mwenyekiti wa mkutano Mh. Shukuru Kawambwa (Waziri wa Elimu) alimtangaza ndugu Mwaking'inda kuwa mshindi wa nafasi ya makamo mwenyekiti kamati tendaji.


KATIBU KAMATI TENDAJI


Kama ilivyo kwa mwenyekiti, naye Katibu wa zamani alipewa dhamana kwa mara nyingine na wajumbe, na matokeo yakawa hivi; 

Mwanaamina Kombakono kura 47, ndugu J. kanumba kura 33, Angelius Liganga kura 18, Khamis .S. khamis kura 10, Hemerick Bambo kura 7 na kura 2 zilihalibika.

Mwenyekiti wa mkutano alimtangaza Bi. Mwanaamina Kombakono kuwa Katibu wa kamati tendaji.


WAJUMBE NANE WA KAMATI TENDAJI


Katika nafasi hii, kuna wajumbe wa awali waliotetea nafasi zao na wengine wapya kushinda nafasi hizo, matokeo yalikuwa mazuri kwa hawa;

Tabia Massudi (95), Maulidi .B. Kitenge (85), Victus .S. Stambuli (84), Deogratias Lubuva (82), Annie Faith Kibira (80), wengine waliochaguliwa kuwa wajumbe ni Fatuma .A. Kange (79), Peter Simon Bhokhe (60) na Cleophace Rutta alijizolea kura 56 na kutimiza idadi ya wajumbe 8 wanaohitajika katika kamati tendaji.
Bi. Tabia Massudi

Peter Bhokhe





















Kama ilivyo katika chaguzi, kuna walioudhunika na kulia na kuna wengine waliojutia kuingia katika kinyang'anyiro cha uchaguzi huu. Wawezakuona idadi ya kura walizopata na pengine walikuwemo awali na kushika madaraka mbalimbali katika chama cha Skauti na sasa wamepata kura ngapi..yote ni matekeo ya UCHAGUZI.


Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza kuu wakifuatilia jambo kwa makini