Ijumaa, 22 Novemba 2013

KAMSHINA MKUU ATANGAZA UTEUZI WA MAKAMISHNA WA MIKOA

  • Ndani ya mwezi mmoja wawe wameandaa mapendekezo ya makamishna wa wilaya.

Taarifa kwa vyombo vya habari leo mchana kufuatia kwa Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania MheshimiwaAbdulkarim Shah (Mb) kufanya uteuzi wamakamishna wa mikoa wapya.
Mheshimiwa Abdurkarim Shah (Mb) Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania akitangaza majina ya Makamishna wa Mikoa wapya mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) tarehe 22.11.2013 katika Ofisi za Chama cha Skauti Tanzania, Upanga Dar Es Salaam.

Kufuatia Mkutano Mkuu Maalum wa uchaguzi uliofanyika tarehe 05 Januari 2013, Baraza Kuu la Chama cha Skauti Tanzania lilianzisha hatua za kuwapata viongozi wa chama Kitaifa. Kuanzia wakati huo hadi sasa viongozi mbalimbali wamechaguliwa, wameteuliwa na kuapishwa. Viongozi hao ni pamoja na Skauti Mkuu Mheshimiwa Mwantum Bakari Mahiza (Mkuu wa Mkoa wa Pwani), Mwenyekiti, Makamo Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama Kitaifa.

Katika mtiririko huo wa safu mpya ya viongozi, Kamishna Mkuu Mheshimiwa Abdulkarim E. H. Sahah (Mb) naye alichaguliwa na kuapishwa. Naye kwa mamlaka aliyonayo katika Katiba ya Chama cha Skauti Tanzania aliwateuwa na kuwaapisha Naibu Kamishna Mkuu na Makamishna Wakuu Wasaidizi kumi na wawili (12)

  • UONGOZI MIKOANI NA WILAYANI

 Lengo kuu la chama cha Skauti Tanzania ni kuwatayarisha vijana kwa kuwajenga katika maadili mema ili waweze kuwa waaminifu, wazalendo, rafiki wa wote, watiifu, wachangamfu, waangalifu na kuwa raia safi katika mawazo, maneno na vitendo.
Ili kufikia dhamira hiyo, chama Makao Makuu hakina budi kuueneza na kuusimamia U-Skauti nchini kote. Hili linatekelezwa na kwa Kamishna Mkuu na wawakilishi wake Mikoani na Wilayani.
Kwa mujibu wa Katiba ya Chama cha Skauti Tanzania ya mwaka 1997 Kifungu 6.11 (a) na (b) hawa watamwakilisha Kamishna Mkuu na kuyatekeleza majukumu yao ambayo kimsingi sawa na ya Kamishna Mkuu bali katika himaya zao.  
Kwa mujibu wa Katiba ya Chama cha Skauti Tanzania kifungu 6.5 (e)(vi), Kamishna Mkuu amewateuwa viongozi wa Skauti wafuatao kuwa Makamishna wa Skauti wa Mikoa na wasaidizi wao:-
MKOA: Arusha
Kamishna: Shakirhussein Badruddin
Naibu Kamishna wake: Wilfred James
MKOA: Dar Es Salaam
Kamishna: Abubakari Mtitu
Naibu Kamishna wake: Grace Kado
 
Skauta Abubakar Mtitu alejea tena Kamishna wa Mkoa wa Dar Es Salaam
MKOA:Dodoma
Kamishna: Daktari Swai
Naibu Kamishna wake: Selistine Raphael

MKOA:Geita
Kamishna: Kiracha Nyamsongolo
Naibu Kamishna wake: Marison .S. Gunje
MKOA: Iringa
Kamishna: John Sichone
Naibu Kamishna wake: Lyason Kajembura


MKOA:Kagera
Kamishna: Fr. Process Mutungi
Naibu Kamishna wake: Beda Kyaishozi
MKOA:Katavi
Kamishna: Mrisho Thabiti Kinanda
Naibu Kamishna wake: Selestine Yoachim China
MKOA: Kigoma
Kamishna: Doecles .H. Bigilwa
Naibu Kamishna wake: Eliudi Marwa
MKOA:Kilimanjaro
Kamishna: Hashim Nyari
Naibu Kamishna wake: Habibu .D. Mvungi
MKOA: Lindi
Kamishna: Aloyce Maira
Naibu Kamishna wake: Bakari Kayombo
MKOA: Mara
Kamishna: Yohana Bonyo
Naibu Kamishna wake: Fred Keya
MKOA: Manyara
Kamishna: Basilisa Martin
Naibu Kamishna wake: Khalifa Salehe Mfanya
MKOA: Morogoro
Kamishna: Francis .G. Francis
Naibu Kamishna wake: Mary Mpasa
MKOA: Mtwara
Kamishna: Erasto Nakati
Naibu Kamishna wake: Hassan .M. Mmadi
MKOA: Mbeya
Kamishna: Sadock Ntole
Naibu Kamishna wake: Boniface Dionis
MKOA: Mwanza
Kamishna: Elibarik Mmari
Naibu Kamishna wake: Wande Mwankyara
MKOA:Njombe
Kamishna: Tusiwene Mahenge
Naibu Kamishna wake: Anita Ngole
MKOA: Pwani
Kamishna: Musiba Bebusiba
Naibu Kamishna wake: Esto Joseph Kalale
MKOA: Rukwa
Kamishna: Mohamed Lugoya
Naibu Kamishna wake: Adengula Mwacha
MKOA: Ruvuma
Kamishna: S. .K. Ndunguru
Naibu Kamishna wake: Hamza Basil Bora
MKOA: Simiyu
Kamishna: Kulwa Mtebe
Naibu Kamishna wake: Jumanne Mangoli
MKOA: Shinyanga
Kamishna: Mussa Chama
Naibu Kamishna wake: Peter mgalula
MKOA: Tabora
Kamishna: Erick Nkwera
Naibu Kamishna wake: Kashinde Masamalo
MKOA:Tanga
Kamishna: Lt. Col (Mstaafu) John Mhina
Naibu Kamishna wake: Nassoro Mbajo
MKOA: Singida
Kamishna: Emmanuel Machemba
Naibu Kamishna wake: Juma Sabigoro
 
  • UTENDAJI

Kufuatia uteuzi wa Makamishna hao, taratibu za kuwaapisha na kuwakabidhi waranti na Katiba zitafuata hivi punde. Barua za uteuzi wao zinafuata. Wakati yote haya yanasubiriwa kwa taarifa hii ni ruksa kwao kuanza kazi mara moja. Alisema Mheshimiwa Shah.
  • MAKAMISHNA WA SKAUTI TANZANIA VISIWANI NA WILAYA 

 Kamishna Mkuu mwenye mamlaka ya kuwateua viongozi hawa yupo katika mchakato wa kushauriana na wasaidizi wake. Mara baada ya zoezi hili kukamilika, tangazo rasmi litatolewa.
Mheshimiwa Shah aliendelea kusema, " Kauli mbiu ya Mkutano Mkuu Maalum wa uchaguzi ilikuwa 'UONGOZI IMARA, CHAMA IMARA' alifafanua kuwa, Chama cha Skauti hakina budi kuwa na uongozi imara unaoweza kusimamia maadili ya vijana wetu hapa nchini kuanzia Makao Makuu hadi Vijijini. Ni matarajio ya wadau wote  wa Chama cha Skauti Tanzania kwamba viongozi wote waliochaguliwa, walioteuliwa na watakaoteuliwa wataongoza kwa kuzingatia Katiba na Maadili ya Chama. Aidha wito unatolewa kwa wanachama na marafiki wa Skauti kutoa ushirikiano kwa uongozi uliopo madarakani.
Kamishna Mkuu alimaliza kwa kuwashukuru wanahabari kwa ushirikiano wao.




MKUTANO WA 7 WA MUUNGANO WA WABUNGE SKAUTI DUNIANI

Mwenyekiti wa Umoja wa Skauti Wabunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Abdulkarim Ismail Shah amechaguliwa kuwa Mweka Hazina Mkuu wa Umoja wa Wabunge Skauti wa Dunia (WPSU)

walishiriki katika Mkutano Mkuu wa Sita wa Umoja wa Skauti Wabunge Duniani ambao unajumla ya nchi wanachama zaidi ya 50. Mkutano huo ulifanyika sambamba na uchaguzi wa viongozi wapya, uliofanyika mjini Tokyo Japan kuanzia Novemba Sita hadi Novemba Nane mwaka huu ambapo Tanzania iliwakilishwa na Mheshimiwa Shah na wabunge wengine watano pamoja na Katibu wa Bunge Umoja wa Wabunge Skauti Tanzania ndugu James John Warburg.

Wabunge wengine waliokuwemo kwenye ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano huo ni Mhe. Gosbert Blandes, Mhe Livingstone Lusinde, Mhe. kuruthum Mchuchuli na Mhe. Lucy Mayenga ambaye ni Makamo Mwenyekiti wa Umoja wa Skauti Wabunge wa Tanzania.

Katika uchaguzi huo ndugu Ryu Shionoya wa Japan amechaguliwa kuwa Rais mpya wa Umoja huo, na makamo wa kwanza wa Rais ni Bi. Ewa thalen Finne kutoka Sweden na makamo wa Rais wa pili ni ndugu Sutham Phanthusak kutoka Thailand.

Akizungumza na wandishi wa habari katikauwanja wa kimataifa wa ndege wa Mwalim Julius Kambarange Nyerere mara baada ya kuwasili kutoka japan, Mheshimiwa Shah amewashukuru wabunge wenzake kwa kumpigiania hadi kushinda kwenye nyadhifa hizo kubwa duniani na kwamba ushindi alioupata ni zawadi kwa Watanzania wote.

Amesema kuchaguliwa kwake kwenye nafasi hiyo ni heshima kwa Tanzania na kwamba ni ushindi kwa Tanzania na kuonyesha kuwa Tanzania inaweza kutoa viongozi katika kuongoza mashirika au taasisi mbalimbali Ulimwenguni, pia mbunge Mvumi Mtera  Mhe. Lusinde alisisitiza kuwa ushindi huo pia umechangiwa na amani iliyopo Tanzania na kwa ushindi huo Tanzania imetangazika katika sekta ya Utalii na kujulikana kijiografia. Aliendelea kusema, "Uchaguzi huo uliohusisha mataifa zaidi ya 50 ulitawaliwa na ushindani mkali, lakini mgombea wa Tanzania alijieleza kwa ufasaha zaidi na vizuri kuwashawishi wajumnbe kumpigia kura na kushinda nafasi hizo.

Mkutano huo mkuu pia ulijadili na kupitisha mabadiliko ya Katiba ambapo muda wa kufanya mkiutano huo umeongezeka kutoka miaka mitatu hadi miaka minne.

Aidha kwamba kuwepo kwenye safu mpya ya uongozi wa Umoja wa Wabunge Skauti wa Dunia utamwezesha kuendeleza vijana kwa kuwapa elimu, ujuzi ili waweze kuajiliriwa au kujiajiri kwa ajili ya maendeleo yao wenyewe na kuondokana na umasikini. Alisema Mhe Shah. 

Mbunge wa Karangwe Mhe. Gosbert Blandes amesema kwamba mkutano huo umemalizika kwa mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kujifunza namna vyama vya Skauti vinavyoendeshwa duniani, ameendelea kusema kuwa 'nchi nyingi duniani wanachukulia Skauti kama chanzo cha elimu na ajira kwa vijana hivyo wao kama wabunge wataishawishi Serikali kutenga fedha za kutosha kwa ajili ya kusaidia uendeshaji wa shughuli za Skauti nchini.

Wakati huo huo Mkutano wa tisa wa wabunge Skauti duniani unatarajia kufanyika nchini Tanzania katika kipindi cha miaka minne ijayo.

Kikubwa yaliyozungumziwa katika mkutano huo ni:
  • Umuhimu wa kuweka mazingira salama kwa watoto kielimu.
  • Umuhimu wa kuwaandaa na kuwapa fursa vijana kuwa viongozi wa baadaye.
  • Majukumu mbalimbali ambayo Wabunge wanaweza kuyatekeleza kwa ajili ya kuwasaidia vijana na Chama cha Skauti.