Jumapili, 30 Desemba 2012

Happy New Year 2012

Every  Scout Leader & Commissioner, wish you a most enjoyable Christmas 2012 and the Year 2013 filled with joy and achievement
Remember, when making your resolutions, resolve to give your Cubs & Scouts an even greater fun & adventure experience than they had in the past year.

Jumapili, 23 Desemba 2012

Ijumaa, 21 Desemba 2012

Dar Es Salaam Local Scouts Association "Inawatakia Furaha ya Krismasi 2012 na Heri ya Mwaka Mpya 2013"

Ijumaa, 30 Novemba 2012

TANGAZO - WAGOMBEA SKAUTI MKUU

Pakua Fomu ya Vigezo na Wagombea wa Skauti Mkuu kwa kubonvya Hapa!! http://www.facebook.com/groups/171718552973513/

Jumamosi, 11 Agosti 2012

Skauti wa Kiislam wafuturisha

 
Sheikh Yakub Bakari toka masjid Shahadhir Kinyerezi-Tabata akitoa mawaidha
Skauti wa Tanzania na wa Finland kwa pamoja wakifuturu
Skauti na waumini wengine wakisikiliza mawaidha
Skauti wa Kiislam Mkoa Dar-Es-Salaam wakiwa katika ghafla ya kufuturisha katika mwezi wa Ramadhani tarehe 11 Agosti 2012 katika viwanja vya Makao Makuu ya Skauti Upanga Dar Es Salaam

Ajali ya MV Skagit

Skauti wakiwa na vikosi vingine vya uokoaji wakielekea Chumbe Unguja kwa ajili ya uokoji wa ajali ya meli ya MV Skagit iliyozama tarehe 18 mwezi wa Saba mwaka 2012.

Jumatano, 23 Mei 2012

Mwenge wa Uhuru

SKAUTI WILAYA YA ILALA WASHIRIKI KUUPOKEA MWENGE WA UHURU
Skauti wilaya ya Ilala wakiwa pamoja na wakimbiza Mwenge katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kutoka wilaya ya Temeke kwenda wilaya ya Ilala tarehe 26/06/2012 eneo la Stesheni ya TaZara, Dar Es Salaam.
 Skauti wilaya ya Iala wakiwavisha skafu wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa katika viwanja vya Stesheni ya TaZara, Dar Es Salaam.
 Mkuu wa wilaya ya Temeke Mh. Sophia Mjema akimkabidhi Mwenge wa Uhuru mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Raymond Mushi tarehe 26/06/2012 katika eneo la Stesheni ya TaZara, Dar Es Salaam.



SKAUTI WILAYA YA ILALA WAENDESHA MAFUNZO YA UONGOZI WA KIKOSI  
PATROL LEADER COURSE- (PEER EDUCATOR TRAINING)
Wahitimu wa mafunzo ya uongozi wa kikosi wilaya ya Ilala wakionyesha vyeti vyao baada ya kuhitimu mafunzo hayo katika viwanja vya makao makuu ya Skauti Dar Es Salaam. Mafunzo hayo yalianza tarehe 22/06/2012 mpaka 24/06/2012.
Kamishina wa Skauti Mkoa wa Dar-Es-Salaam Abubakar Mtitu (aliyevaa fulana ya mistari) akiwapa maelekezo ya mchezo wa kuonyesha umuhimu wa kutunza kumbukumbu washiriki wa mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo wakisikiliza jambo
Baadhi ya washiriki wa mafunzo wakiwa katika hema wakibadilishana mawazo juu ya mafunzo ya uongozi wa kikosi
 Scouts Life Saving Activity

 
Sherehe ya kuapishwa kwa Skauti Mkuu Kanali mstaafu .O. Kipingu Ikulu jijini Dar es Salaam, mwaka 2008.
Mlezi  wa Skauti Tanzania Mhe. Dkt Jakaya .M. Kikwete (Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (aliyevaa suti nyeusi). Wa kwanza kulia ni Makamo wa Rais Tanzania Mhe. Ali .M. Shein, [kulia kwa rais ni mkufunzi wa Chama cha Skauti Tanzania ndugu Ngunga.


Naibu Waziri wa Elimu, Mhe. Mwantumu Mahiza aliyevaa kofia ya kijani akibadilishana mawazo na wajumbe wa mkutano wa Skauti wa nchi za Afrika Mashariki mjini Morogoro katika kambi ya Bahati, mwaka 2008.