Jumamosi, 18 Mei 2013

TANZIA TANZIA TANZIA

Maskauti wakiwa wamezunguka Sanduku la Marehemu Emmanuel Peter Ndungwi wakiwa katika Kanisa Katoriki, Tegeta katika Misa ya kumuombea marehemu tarehe10 Mei, 2013

Marehemu Emmanuel Peter













Chama cha Skauti Tanzania kimepata msiba wa mwanachama wake Marehemu Skauti Emmanuel Peter Ndungwi aliyefariki tarehe 9 Mei, 2013 katika hospitali ya Temeke Dar Es Salaam, Kwa mujibu wa taarifa ya kiongozi wake wa kundi la Skauti la St. Mary Morogoro Skauta Omari Juma alisema, Marehemu Emmanuel alizaliwa tarehe 22 Aprili, 1999 uko Dodoma na kusoma katika shule ya msingi St. Mary's mkoani Morogoro hadi kifo kinamfikia akiwa darasa la sita.

WASIFU WA MAREHEMU

Kwa mujibu wa dada wa marehemu Bi. Veronica Ndungwi amesema, marehemu Emmanuel alibatizwa mwaka 2003 mkoani Kigoma katika Parokia ya Mt. Ceccilia, alipata Komonio ya kwanza pamoja na Kipa Imara mwaka 2012 katika Parokia ya Kihonda Mkoani Morogoro. Marehemu alitumikia Kanisa kama muhudumu wa Altare ya bwana.
Marehemu alijiunga na Skauti tarehe 14 Machi, 2011 hadi anafariki alikuwa mwanachama wa Skauti. Alishiriki katika kambi na mafunzo mbalimbali na kambi yake ya mwisho ilikuwa tarehe 13 hadi 16 Februari 2013 iliyofanyika katika Kambi la Taifa ya Skauti (BAHATI CAMP) Mjini Morogoro .

Marehemu Emmanuel alianza kuumwa tarehe 29 Aprili, 2013 na alifariki tarehe 9 Mei, 2013 katika hospitali ya Temeke jijini Dar Es Salaam baada ya kuugua ugonjwa wa Maralia na Homa ya matumbo (Taifodi)