Chama cha SKAUTI Tanzania kinakaribisha maombi ya kugombea nafasi ya KAMISHINA MKUU.
Katika kikao chake cha Viongozi waandamizi (Skauti Mkuu, Kamati Tendaji, Kamati ya Mpito na Wakufunzi) kilichofanyika tarehe 09 Mei, 2013 chini ya Uenyekiti wa Skauti Mkuu Mh. Mwantum Mahiza kimeazimia mambo yamsingi yafuatayo:-
- · Kutangaza
kimaandishi nafasi iliyowazi ya Kamishna Mkuu.
Hii ni nyongeza ya tangazo alilolitoa Skauti Mkuu katika Mkutano wake na
viongozi mbali mbali jijini Dar es
Salaam uliofanyika tarehe 06 Mei 2013.
- · Kutoa
sifa na fomu za kugombea.
Sifa na Fomu za kugombea nafasi hiyo zinatolewa Makao Makuu ya
Chama kuanzia tarehe 10 Mei, 2013.
-
Kwa “Despatch” kwa Mwenyekiti au Karani wake, Makao Makuu ya Chama.
-
Kwa “Registered Mail – Mwenyekiti wa Kamati ya mpito, Chama cha
Skauti Tanzania S.L.P 945 DSM.
Mwisho wa kurejesha fomu ni
tarehe 20 Mei 2013, saa 10.00 jioni.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Mpito Brigedia Jenerali Mstaafu Gerald Mkude, ameelezea sifa za mwombaji wa nafasi hiyo ni:-
1.
Awe Kamishna au aliwahi kuwa Kamishna
2.
Awe Mtanzania
3.
Awe hajawahi kuachishwa uongozi katika Chama cha Skauti au
kushitakiwa kwa makosa ya jinai kwa kipindi cha miaka minne (4) iliyopita.
4.
Awe ametunukiwa Nishani ya Skauta (Woodbadge Holder)
5.
Awe na Elimu ya Sekondari au zaidi.
6.
Awe na uzoefu wa uongozi na utawala katika shughuli za Skauti na
jamii kwa ujumla kwa muda usiopungua miaka 5.
7.
Awe ametoa mchango mkubwa wa huduma kwa Chama cha Skauti na jamii
kwa ujumla.
8.
Awe ana uwezo wa kusimamia, kulinda na kutetea Katiba na Kanuni za
Skauti wakati wote.
9.
Awe mtu wa kujiamini na kujitambua.
10.
Awe mweledi na mwaminifu
11.
Awe na uwezo wa mawasiliano Kitaifa na kimataifa.
12.
Awe mwenye umri wa miaka 35 au zaidi
Mwombaji atajaza Fomu iliyotayarishwa,
pia alete maelezo yake binafsi yaani C.V. yake.
Fomu hiyo ipo katik utaratibu ufuatao:-
FOMU YA KUGOMBEA NAFASI YA
KAMISHNA MKUU
FOMU NO: …………..
SEHEMU (A): MAELEZO BINAFSI (HERUFI KUBWA)
1. JINA KAMILI ……………………………………………………………….
2. UMRI …………………... MAKAZI ……………………………
3. ELIMU ………………………………………………………………………….
4. KAZI ………………………………… MAHALI
………………………
5. ANUANI YA POSTA ……………………………………………………
6. SIMU …………………… EMAIL ………………………………………
- UZOEFU WA UONGOZI
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
- SAHIHI ………………………………………………….
SEHEMU (B): MAONI YA KIKAO CHA UCHAMBUZI
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
SAHIHI YA
MWENYEKITI/KATIBU……………………………….. TAREHE …………….
SEHEMU (C): MATOKEO YA UCHAMBUZI
………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………
SAHIHI YA
MWENYEKITI/KATIBU………………………………..
TAREHE ……………………
Mwisho wa kurejesha fomu ni
tarehe 20 Mei 2013, saa 10.00 jioni.