Ijumaa, 12 Julai 2013

KAMISHNA MKUU AAPISHWA

  • Safu ya Uongozi ya Skauti yaanza kukamilika
    • Gerald Mkude ateuliwa kukaimu Kamishna Mtendaji 
Chama cha Skauti Tanzania kimeweka historia nyingine baada ya kuapishwa kwa Kamishna Mkuu mpya kwa mwaka 2013 - 2016.
Skauti Mkuu Mhe. Mwantum Mahiza (Mkuu wa Mkoa wa Pwani) akimwapisha Kamishna Mkuu (hayupo katika picha) tarehe Julai 12, 2013 katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, mjini Kibaha.


Mhe. Abdulkarim Shah (Mbunge wa Mafia na Mwenyekiti wa  Kikundi cha Skauti wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) akiapa kuwa Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania, tarehe Julai 12, 2013 katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, mjini Kibaha.
Skauti Mkuu Mhe. Mahiza akisaini Kiruhusishi (Warrant) baada ya kumuapisha Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania, tarehe Julai 12, 2013 katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, mjini Kibaha.

Skauti Mkuu Mhe. Mwantum Mahiza (kulia) akisalimiana na Kamishna Mkuu Mhe. Shah baada ya kuapishwa kuwa Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania, tarehe Julai 12, 2013 katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, mjini Kibaha.

Skauti Mkuu Mhe. Mwantumu Mahiza (Mkuu wa Mkoa wa Pwani) amemuapisha Mhe. AbdulKarim Shah (Mbunge wa Mafia na Mwenyekiti wa Kikundi cha Skauti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) kuwa Kamishna Mkuu. Mhe. Shah aliongoza kwa kura nyingi katika uchaguzi uliofanyika siku ya Jumamosi tarehe 06 Julai, 2013 katika ukumbi wa makao makuu ya Skauti jijini Dar es Salaam.

Katika uchaguzi huo ambao ulikuwa na wagombea wapatao 9. Idadi ya Kura na majina ya wagombea hao ni Mhe. AbdulKarim Shah (24), Faustin Magige, Rashidi Mchata (19), Hamisi Masasa (11), Mathusela Magoti (3) wengine ni Pharas Magesa (19), Osmundi Kipengele (4), Lawrence Muhomwa (8) na Frank Msina (5).

Kuelekea katika uchaguzi huo, Kamishna Faustin Magige alijiengua katika kinyang'anyiro hicho na kufanya kubakia wagombea 8.
 
Mhe. Shah alipata idadi ya kura nyingi, akifuatiwana Rashidi Mchata na Pharas Magesa kwa kufungana kwa kura. 

Skauti Mkuu Mhe. Mwantum Mahiza (kushoto) katika picha ya pamoja na Kamishna Mkuu Mhe. Shah baada ya kuapishwa Kamishna Mkuu tarehe Julai 12, 2013 katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, mjini Kibaha.

Skauti Mkuu Mhe. Mwantum Mahiza (katikati) katika picha ya pamoja na Kamishna Mkuu Mhe. Shah (kushoto) na kulia ni Gerald Mkude (Kaimu Kamishna Mtendaji) baada ya kuapishwa Kamishna Mkuu tarehe Julai 12, 2013 katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, mjini Kibaha.

Kamishna Mkuu Mhe. Shah (kulia) katika picha ya pamoja na ndugu James .J. Warburg Katibu wa Kikundi cha wabunge Skauti wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya shughuli za Bunge - Bunge la Tanzania, tarehe Julai 12, 2013 katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, mjini Kibaha.
 Katika hotuba fupi baada ya kumuapisha Kamishna Mkuu, Skauti Mkuu Mhe Mwantumu Mahiza alisema "hatua ya pili ya mchakato wa uongozi wa Skauti Tanzania umekamilika leo" 
Katika hotuba hiyo Skauti Mkuu alisisitiza kuwa Chama cha Skauti ni cha kujitolea na si cha mtu binafsi au kikundi cha watu fulani, uongozi huu kwa kushirikiana na kamati tendaji kuna kazi kubwa ya kuimarisha chama, kurejesha imani na marafiki na kukijengea chama heshima inayostahili, Skauti Mkuu aliendelea kusema, "Katika kufanya hivyo na kufikia malengo, kuna watu ambao watakaoachwa katika madaraka yao waliokuwa nayo sasa ama kuachia wenyewe na kubakia kuwa wanachama wa kawaida wa chama cha Skauti Tanzania"

Pia Skauti Mkuu Mhe. Mahiza alisisitiza Skauti kuzingatia weledi na heshima na kuondoa umimi katika chama. Alitumia nafasi hiyo pia kuwaomba radhi kwa wale watakao guswa na kuachwa katika nafasi mbalimbali za uongozi wa chama na kuacha chama kiendelee. Mwisho Mhe. Mahiza alisema "Simchukii mtu naomba tupishane ili kujenga chama cha Skauti"

Skauti Mkuu Mhe. Mahiza, alimteua Gerald Mkude (aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya mpito) kuwa Kaimu Kamishna Mtendaji mpaka hapo  atakapopatikana kamishna mtendaji wa kuajiriwa.
Kamishina wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Abubakar Mtitu (kushoto) na Juma Massudi (Kulia) ni baadhi ya Viongozi waliohudhulia kuapishwa kwa Kamishna Mkuu tarehe Julai 12, 2013 katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, mjini Kibaha.

Hamisi Masasa Kamishna wa Mkoa wa Pwani (kushoto) na Faustin Magige (kulia) baadhi ya Viongozi waliohudhulia kuapishwa kwa Kamishna Mkuu tarehe Julai 12, 2013 katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, mjini Kibaha.
Katika salamu zake za kushukuru Mhe. Shah alisisitiza kuwa na umoja, kuondoa makundi na kuweka mshikamano kwa maendeleo ya wote huku akisisitiza kufuata katiba, kanuni na ahadi ya chama cha Skauti Tanzania.

"Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuwepo na kupata nafasi hii katika chama cha Skauti Tanzania, nitafuata katiba, kanuni na ahadi ya Skauti katika kutekeleza majukumu yangu haya" alisema Mhe. Shah.

Pia alisisitiza kuheshimu kila mtu bila ya kuangalia umri, kulinda heshima kwa kila mmoja pamoja na kushirikiana na kamati tendaji, Skauti na viongozi wengine kwa busara na kufanyakazi kwa uwezo wake katika kuleta na kusimamia mabadiliko ya maendeleo katika chama.
Viongozi waliohudhulia kuapishwa kwa Kamishna Mkuu tarehe Julai 12, 2013 katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, mjini Kibaha.
Skauti Mkuu Mhe. Mahiza (wa tano kutoka kulia), mwenyekiti wa kamati tendaji Balozi Kuhanga (wa nne kutoka kushoto), Kamishna Mkuu Mhe. Shah (kulia mwa Skauti Mkuu) katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa kamati tendaji na viongozi wengine wa Skauti, tarehe Julai 12, 2013 katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, mjini Kibaha.

SKAUTI MKUU APOKEA ZAWADI

Katika hali iliyomshangaza Skauti Mkuu Mhe. Mwantum Mahiza ni zawadi alizopokea kutoka kwa Kamishna wa Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam Abubakar Mtitu kwa niaba ya Skauti Tanzania. Zawadi hizo ni picha kubwa ya taswira yake iliyochorwa na kinyago cha twiga, wakimtakia utendaji mzuri wa uongozi wake ikiwakama ishara ya wasifu wa mnyama huyo.
Skauti Mkuu Mhe. Mwantum Mahiza (kushoto) akionyesha zawadi mojawapo waliyopewa pembeni yake ni Kamishna Mkuu Mhe. Shah. Tarehe 12 Julai, 2013 katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, mjini Kibaha.
Kamishna wa Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam Abubakar Mtitu akimkabidhi moja ya zawadi Skauti Mkuu Mhe. Mwantum Mahiza. Tarehe 12 Julai, 2013 katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, mjini Kibaha.