- NAIBU KAMISHNA MKUU AAPISHWA
Chama cha Skauti Tanzania chazidi kukamilisha safu ya viongozi wake wa juu.
Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mlezi wa Skauti Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kumteuwa na kumuapisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani ambaye ni Skauti Mkuu Mhe. Mwantumu Mahiza, nawe Skauti Mkuu alimuapishwa Kamishna Mkuu kwa kufuata katiba na kanuni za Skauti.
Katika hali ya kutaka kuhakikisha chama kinakuwa na mwelekeo mzuri na kurudisha heshima kwa kufuata kanuni na katiba ya Skauti, Kamishna Mkuu amemteua na kumuapisha Naibu Kamishna Mkuu Rashid Kassim Mchatta, tarehe Julai 19, 2013 katika ofisi za Makao Makuu ya Skauti Tanzania Upanga, jijini Dar Es Salaam.
Kiruhusishi (Warrant) cha Naibu Kamishna Mkuu Rashid Mchatta |
Picha ya pamoja Kamishina Mkuu pamoja na baadhi ya viongozi wa Skauti waliohudhuria kuapishwa kwa Naibu Kamishna Mkuu. |