Chama cha Skauti Tanzania kipo katika majonzi makubwa baada ya kufikwa na msiba wa Skauti pamoja na kufiwa kwa wazazi wa baadhi ya Skauti.
Marehemu Skauta Frank Msina amefariki dunia tarehe Julai 16, 2013.
Marehemu Skauta Frank Msina enzi za uhai wake |
Marehemu Frank Msina wakati wa uhai wake aliwahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi katika Chama cha Skauti Tanzania.
Wasifu wa marehemu kwa mujibu wa mahojiano kwa njia ya simu na mkufunzi wa Skauti, Skauta Stewart Kiluswa alisema, "marehemu Msina mwaka 1977 alikuwa Skauti katika kundi la Shule ya Sekondari ya Shabani Robert jijini Dar Es Salaam, kati ya mwaka 1978 na 1979 alikuwa kiongozi msaidizi wa kundi la Shule ya Msingi Makulumla na Karume jijini Dar Es Salaam, mwaka 1998 mpaka 2000 alikuwa Naibu Kamishna wa Skauti wa Mkoa wa Dar Es Salaam, 2000 mpaka 2001 alishika nafasi ya uongozi ya Kamishna wa Mkoa wa Dar Es Salaam. Mwaka 2001 hadi 2010 aliishi nchini Uingereza. Marehemu Msina alikuwa miongoni mwa wanachama wa Skauti Tanzania waliogombea nafasi ya Kamishna Mkuu mnamo tarehe Julai 06, 2013"
Msiba upo nyumbani kwa marehemu Gongo la Mboto, Kipunguni. Marehemu Frank Msina atazikwa tarehe Julai 20, 2013 katika makaburi ya Buguruni Malapa saa saba mchana.
Pamoja na msiba huo, baadhi ya skauti waliofikwa na msiba ni Skauta Osimundi Kipengele, ambaye amefiwa na baba yake mzazi Mzee Andrea Mchumo Kipengele.
Marehemu Mzee Kipengele amefikwa na mauti alfajiri ya tarehe Julai 18,
2013 nyumbani baada ya kulazwa na kuruhusiwa kutoka katika hospitali ya
Taifa ya Muhimbili alipolazwa. Msiba upo nyumbani kwa Osimundi Kipengele
Yombo Machimbo, mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa Mkoani Lindi
tarehe Julai 19, 2013 na mazishi yatafanyika Kilwa Kipatimo siku ya
Jumamosi tarehe Julai 20, 2013 katika hosipitali ya Taifa ya Muhimbili
alipokuwa amelazwa.
Msiba mwingine ni wa baba wa mlinzi wa makao makuu ya Skauti ndugu Ally Masisi ambaye amefiwa na baba yake mzazi Mzee Masisi.
Marehemu Mzee Masisi amefikwa na mauti tarehe Julai 17, 2013 katika hosipitali ya Taifa ya Muhumbili mjini Dar Es Salaam. Msiba upo nyumbani kwa marehemu Mbagala. Mazishi yatafanyika Mkamba, Kisarawe tarehe Julai 18, 2013.
Skauti wote tunaombwa kuhudhuria na kutoa rambirambi zetu kwa wafiwa.
Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi...AMINA.