Mheshimiwa Mwantum Mahiza, Skauti Mkuu |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Skauti Tanzania, amemteua Mh. MWANTUM Bakari Mahiza kuwa Skauti mkuu wa chama cha Skauti Tanzania.
Kwa mujibu wa barua ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amesema uteuzi wa mheshimiwa Mahiza umeanza tangu tarehe 19 Aprili 2013, kwa uteuzi huo mheshimiwa Mahiza anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Kanali mstaafu Iddi Kipingu ambaye amemaliza muda wake.
Mh. Mahiza ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, aliibuka na kura 47 katika mkutano mkuu wa baraza kuu la Skauti nchini tarehe 05 Januari 2013 katika ukumbi wa Dob Bosco jijini Dar Es Salaam.
Habari hii kwa mujibu wa :
KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI