Alhamisi, 18 Aprili 2013

Hati ya Shukrani

Hati hii ya shukrani kwa Skauti Tanzania imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar-Es-Salaam kwa kuthamini mchango wao katika kuhudumia jamii.

Skauti wamekuwa na utamaduni wa kusaidia, kufundisha na kuelimisha mambo ya msingi kwa jamii .  Desturi hii ya Skauti inadhiirika pale wanapokuwa mstari wa mbele katika kuchangia elimu isiyokuwa rasmi, kufundisha maadili yaliyo bora na mema kwa jamii. Skauti wamekuwa wakisaidia, kutoa huduma ushahuri kwa waliokumbwa na maafa, tarehe  31/03/2013 Skauti walishiriki uokoaji wa jengo lililo "poromoka" lililokuwa mtaa wa Indira Ghandi na barabara ya Morogoro jijini Dar Es Salaam.


Kamishina wa Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam, Kamishina Abubakari Mtitu akipokea hati ya shukrani toka kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa, tarehe 07/02/2013 kwa kutambua mchango wa Skauti Tanzania katika kuhudumia waanga wa mafuriko yaliyotokea tarehe 20/12/2011 kwenye kata ya Upanga Magharibi jijini Dar Es Salaam.

Picha ya pamoja Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry W. Silaa wa pili toka kulia (aliyevaa suti na tai), Diwani wa Kata ya Upanga Magharibi Mh. Mbaga wa pili toka kushoto, kamishina wa Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam Kamishina Abubakari Mtitu aliyeshika hati ya shukrani (aliyesimama katikati) pamoja na viongozi wa Makundi ya Skauti, Rajabu Mpita wa kwanza kushoto na wa kwanza kulia ni ndugu Ally.


Hakuna maoni: