Jumatatu, 5 Februari 2018

Skauti na Vitambulisho

Chama cha Skauti Tanzania baada ya kuendeleza mchakato wa kuwa na mfumo mzuri wa kutunza kumbukumbu za wanachama wake hatimaye sasa wajikomboa.
Mchakato huo ambao ni pamoja na kuwa na kitambulisho au kadi ya mwanachama madhubuti ulianzia tangu mwaka 2015.

[ Ndugu Sabasaba Moshingi Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB bank (kulia) na ndugu Abdulkarim Shah Kamishna Mkuu wa Skauti (kushoto) wakisaini mkataba wa ushirikiano leo tarehe 23 Januari 2018 katika ofisi ya Makao Makuu ya TPB bank, Dar es Salaam[/caption]
Hatimaye leo (23 Januari, 2018) Chama cha Skauti Tanzania kimefanikisha na kuweza kusaini mkataba na Benki ya Posta Tanzania.
Mkataba ambao utawezesha TSA kuwa na “database” ambayo itaweza kuhifadhi kumbukumbu ya mwanachama na kuweza kukusanya ada za mwanachama kwa uhakika zaidi.
“Naweza kusema kuwa ni mfumo wa kwanza kwa Skauti duniani kote, Tanzania tumeonyesha njia bora ya kujua idadi ya wanachama na kwa njia hii” alisema Shah Kamishna Mkuu.

Benki ya Posta wafarijika

Ndugu Sabasaba Moshingi Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania alisema benki yao imefarijika sana kwa kushirikiana na Chama cha Skauti Tanzania katika mfumo huu wa kuwezesha mwanachama wa Skauti kuwa na akaunti pamoja na kutumia kadi yake ya benki kama kitambulisho kitakacho weza kuweka kumbukumbu zake.
Ndugu moshing ameyataja baadaadhi ya manufaa yatakayopatikana kwa Skauti kuwa ni kuwezesha TSA kuwa na “database” ya wanachamwa wake, kuwa na kitambulisho cha kisasa chenye kuweka kumbukumbu na pamoja kumwezesha mwanachama kuwa na akaunti yenye kuwezesha kulipia ada yake ya uanachama kwa urahisi zaidi.
TPB bank inajumla ya matawi 68 makubwa na madogo. Ndugu Moshingi alisema wamejipanga kikamilifu na kuweza kufungua “online” kwa njia ya mtandao popote pale utakapokuwa, na huduma zake ni rahisi waweza kutumia mitandao ya simu kuweka akiba yako.
] Ndugu Sabasaba Moshingi Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB bank akibadilishana mkataba wa mahusiano na ndugu Abdulkarim Shah Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania, wa kwanza kushoto ni ndugu Juma Massudi Kamishna Mkuu Msaidizi idara ya Hati na Usajili Chama cha Skauti Tanzania akishuhudia.



Ndugu Sabasaba Moshingi Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB bank na ndugu Abdulkarim Shah Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania wakionyesha mfano wa Kitambulisho cha Skauti pia ni Kadi ya benki.

Balozi Kuahanga naye:

Balozi Nicolaus Kuhanga Mwenyekiti wa Kamati Tendaji Chama cha Skauti Tanzania hakuficha furaha yake na kusema kuwa “ushirikiano huu utaleta maendeleo kwa TSA” aliendelea kusema kuwa mfumo huu utawezesha TSA kuweza kukusanya ada kiukamilifu na bila kificho.

Massudi meno 32 nje

Jambo hili limemfurahisha sana ambalo lipo katika idara yake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni