VIONGOZI WA CHAMA CHA SKAUTI TANZANIA WAKUTANA NA BALOZI SONG.
Baadhi ya viongozi wa Chama cha Skauti Tanzania leo wamekuwa na mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Korea.
Viongozi hao waliongozwa na Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania Ndugu Abdulkarim Shah.
Kwa habari zilizotufikia ni kwamba, Skauti walipata mwaliko na Balozi huyo na kutaka kuzungumza juu ya maendeleo na ushirikiano baina ya Jamhuri ya Korea na Skauti Tanzania.
Viongozi hao wa Skauti katika mahojiano na mwandishi wetu walisema kuwa wamefurahi kupata mwaliko huo na wanatumaini kuwa utakuwa ni mazungumzo hayo yatafungua mahusiano ya kimaendeleo baina ya Tanzania na Jamhuri ya Korea kwa upande wa vyama vyao vya Skauti.
Mhe. Balonzi Song, Geum-young (kulia) katika picha na Kamishna Mkuu Abdulkarim Shah. Picha hii walipiga muda mfupi baada ya mazungumzo katika ofisi ya Ubalozi wa Jamhuri ya Korea. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni