|
MUDA
|
TUKIO
|
MHUSIKA
|
|
Saa 3:00 Asubuhi
|
Skauti kuwasili Uwanja wa Taifa
|
Skauti wote
|
|
Saa 3:30 Asubuhi
|
Maandamano kuelekea viwanja vya Mwl.
Nyerere, Saba Saba
|
Skauti na Viongozi wao
|
|
Saa 3:30 Asubuhi
|
Ø
Viongozi wa Chama kuwasili Ukumbini.
Ø
Skauti Mkuu na Mwenyekiti Kamati Tendaji(T) kuwasili ukumbini.
Ø
Wageni waalikwa kuwasili ukumbini.
|
Kamati ya Mapokezi/ MC
|
|
Saa 4:00 Asubuhi
|
Mgeni Rasmi kuwasili Uwanjani na kuvishwa
Skafu.
Ø Mgeni Rasmi
kupokea maandamano.
|
Kamishna Mkuu,
Naibu Kamishna Mkuu,
Kamishna wa Mkoa(DSM)
Kamishna Mtendaji,
|
|
Saa 4:05
Asubuhi
|
Mgeni Rasmi kuingia Ukumbini.
Ø Wimbo
maalum (Twamkumbuka Mzee wetu Baden Powell)
Ø Utambulisho
wa wageni maalum
|
Skauti wote
Kamishna Mkuu
|
|
Saa 4:15
Asubuhi
|
Nasaha za Skauti Mkuu
|
Skauti Mkuu
|
|
Saa 4:30 Asubuhi
|
Burudani
|
MC
|
|
Saa 4:40 Asubuhi
|
Uzinduzi wa Mpango Mkakati
(Strategic Plan 2014 – 2017)
|
Mgeni Rasmi,
Kamishna Mkuu Msaidizi Miradi.
|
|
Saa 4:50 Asubuhi
|
Kuapishwa
kwa Makamishna wa Mikoa
Ø Burudani.
|
Kamishna Mkuu
Skauti.
|
|
Saa 5:20 Asubuhi
|
Kuwekwa saini kwa Mkataba wa Hifadhi
ya Msitu wa Vikindu
|
Kamishna Mkuu
Mkurugenzi wa Hifadhi ya Misitu
|
|
Saa 5:30 Asubuhi
|
Burudani (Maonesho ya Sanaa ya
mapigano)
|
Kikosi cha Rova
|
|
Saa 5:40 Asubuhi
|
Tukio maalum
|
MC
|
|
Saa 5:50 Asubuhi
|
Nasaha za Mgeni Rasmi
|
Mgeni Rasmi
|
|
Saa 6:00 Mchana
|
Kurudia Ahadi
|
Wote/ Kamishna Mkoa
|
|
Saa 6:05 Mchana
|
Neno la
shukrani
|
Mwenyekiti Kamati Tendaji
|
|
Saa 6:15 Mchana
|
Chakula
|
Kamati ya Chakula
|
|
|
MWISHO
|
|
Dar Es Salaam Local Scouts Association
Jumatano, 19 Februari 2014
RATIBA YA SHEREHE YA SIKU YA MWANZILISHI WA SKAUTI DUNIANI LORD BADEN POWEL - 22 FEBRUARI 2014
Jumamosi, 18 Januari 2014
KAMATI YA UENDESHAJI YA MKOA YATEMA CHECHE
Kuandaa Siku ya kumbukumbu ya Mwanzilishi wa Skauti Duniani
Chama cha Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam kupitia Kikao chake cha Kamati ya uendeshaji kimetoa wito kwa Skauti Mkoa wa Dar es Salaam kujiandaa na siku ya kumbukumbu ya mwanzilishi wa Skauti Duniani (Founder's Day) inayotarajiwa kufanyika kimkoa kuanzia tarehe 21 Februari, 2014 mpaka 23 Februari, 2014.
"Wito unatolewa kufanya kazi za huduma kwa jamii kwa kujitolea kama ilivyo ada na wajibu wa Skauti" alisema Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Kamishna wa Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam Kamishna Abubakar Mtitu. Ndugu Mtitu alisisitiza kuwa Skauti ni watu wenye nidhamu, kujali na kufuata misingi ya utu, kujitoa kwa jamii katika kutekeleza kanuni na ahadi za Skauti.
Pia Kamishna Mtitu alisema mambo waliojadiliana katika kikao hicho ni muhimu sana katika kuendeleza Skauti na wanakamati wamekubaliana kutekeleza maazimio ya kikao hicho.
Mwanyato James ambaye ni Mratibu wa Mafunzo Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam alisema katika mahojiano na waandishi wa habari kuwa "Natumai tutayatimiza yote tuliyoyajadili, pia nafuraha sana kuona kikao hiki kimehudhuliwa na watendaji wakuu wote wa Skauti Wilaya za Dar Es Salaam, naomba tuendelee hivi kwa kasi hii kwa maendeleo ya Skauti na jamii yetu"
Kamati imekubaliana kuandaa siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa Skauti Duniani (Founder's Day), Marehemu Paden Pawell aliyezaliwa tarehe 12 Februari 1857 na kufariki tarehe 8 Januari, 1941.
Mwenyekiti Mtitu alitumia fursa katika kikao hicho kuwatambulisha baadhi ya wajumbe wapya ambao ni James Mwanyato (Mafunzo), Mama Ramadevi Sankran Lyer (Kabu), Sameer Somji (Kazi Maalum), Titto Jackson pamoja na Leonard Gerlad Kiloka (Uakilishi wa Vijana) na wengine ni S. Salim (Mambo ya Nje na uhusiano), Reuben Mlay (Vijana), Anthony Meda (Makambi na Mawasiliano) na Bi Annick Verstraelen (Miradi)
Pia Kamishna Mtitu alisema mambo waliojadiliana katika kikao hicho ni muhimu sana katika kuendeleza Skauti na wanakamati wamekubaliana kutekeleza maazimio ya kikao hicho.
![]() |
| Mratibu Mafunzo wa Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam Ndugu Mwanyato James |
Kamati imekubaliana kuandaa siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa Skauti Duniani (Founder's Day), Marehemu Paden Pawell aliyezaliwa tarehe 12 Februari 1857 na kufariki tarehe 8 Januari, 1941.
Mwenyekiti Mtitu alitumia fursa katika kikao hicho kuwatambulisha baadhi ya wajumbe wapya ambao ni James Mwanyato (Mafunzo), Mama Ramadevi Sankran Lyer (Kabu), Sameer Somji (Kazi Maalum), Titto Jackson pamoja na Leonard Gerlad Kiloka (Uakilishi wa Vijana) na wengine ni S. Salim (Mambo ya Nje na uhusiano), Reuben Mlay (Vijana), Anthony Meda (Makambi na Mawasiliano) na Bi Annick Verstraelen (Miradi)
Ijumaa, 27 Desemba 2013
MASHINDANO YA SKAUTI AFRIKA MASHARIKI NA KATI
- Timu ya Tanzania yakabidhiwa bendera kuipeperusha Burundi
Timu ya Taifa ya Skauti Tanzania imekabidhiwa Bendera ya Taifa na ya Chama cha Skauti Tanzania pamoja na vifaa vyote baada ya kupata mafunzo na mbinu zaidi za Skauti kwenda kushiriki katika mashindano ya Skauti ya Afrika Mashariki na Kati pamoja na kuhudhuria kongamano la Vijana la Skauti nchini Burundi. Timu hiyo inatarajia kuondoka nchini kuelekea Burundi tarehe 29 Desemba 2013 hadi tarehe 04 Januari 2014.
Akikabidhi bendera hizo, Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania Mhe. Shah aliwatakia wawakirishi hao kila la heri na kuwataka Skauti na Watanzania wote kuwaombea mafanikio mema na hatimaye kurudi nyumbani na ushindi. Mheshimiwa Shah alisema, "Ushindi mtakao upata ni wa Tanzania mzima na siyo wa mtu mmoja mmoja, hivyo pamoja na mafunzo na mbinu za Skauti mlizopata, tuna waombea kila lililo la kheri kwa Mwenyezi Mungu mfike salama na mpeperushe vyema bendera ya nchi yetu" aliongeza kwa kusema, "Sisi Skauti na Watanzania wote tupo pamoja nanyi katika safari na katika mashindano hayo, mtuwakirishe vyema"
| Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania Mheshimiwa Shah akikabidhi bendera ya Skauti Tanzania kwa timu ya Skauti itakayoshiriki mashindano ya Skauti ya Afrika Mashariki na Kati nchini Burundi. |
| Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania Mheshimiwa Shah akikabidhi bendera ya Tanzania kwa timu ya Skauti itakayoshiriki mashindano ya Skauti ya Afrika Mashariki na Kati nchini Burundi. |
| Baadhi ya Vijana wa kike wa timu ya Skauti ya Taifa inayokwenda nchini Burundi kwa Mashindano ya Skauti Afrika Mashariki na Kati |
| Baadhi ya Vijana wa kiume wa timu ya Skauti ya Taifa inayokwenda nchini Burundi kwa Mashindano ya Skauti Afrika Mashariki na Kati |
| Baadhi ya vijana wa timu ya Skauti ya Taifa wakionyesha jambo katika viwanja vya Makao Makuu ya Skauti Upanga tarehe 26.12.2013 |
| Baadhi ya vijana wa timu ya Skauti ya Taifa wakiteta jambo katika viwanja vya Makao Makuu ya Skauti Upanga tarehe 26.12.2013 |
| Timu ya Skauti ya Taifa itakayoshiriki mashindano ya Skauti nchini Burundi |
Ijumaa, 22 Novemba 2013
KAMSHINA MKUU ATANGAZA UTEUZI WA MAKAMISHNA WA MIKOA
- Ndani ya mwezi mmoja wawe wameandaa mapendekezo ya makamishna wa wilaya.
Taarifa kwa vyombo vya habari leo mchana kufuatia kwa Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania MheshimiwaAbdulkarim Shah (Mb) kufanya uteuzi wamakamishna wa mikoa wapya.
Kufuatia Mkutano Mkuu Maalum wa uchaguzi uliofanyika tarehe 05 Januari 2013, Baraza Kuu la Chama cha Skauti Tanzania lilianzisha hatua za kuwapata viongozi wa chama Kitaifa. Kuanzia wakati huo hadi sasa viongozi mbalimbali wamechaguliwa, wameteuliwa na kuapishwa. Viongozi hao ni pamoja na Skauti Mkuu Mheshimiwa Mwantum Bakari Mahiza (Mkuu wa Mkoa wa Pwani), Mwenyekiti, Makamo Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama Kitaifa.
Katika mtiririko huo wa safu mpya ya viongozi, Kamishna Mkuu Mheshimiwa Abdulkarim E. H. Sahah (Mb) naye alichaguliwa na kuapishwa. Naye kwa mamlaka aliyonayo katika Katiba ya Chama cha Skauti Tanzania aliwateuwa na kuwaapisha Naibu Kamishna Mkuu na Makamishna Wakuu Wasaidizi kumi na wawili (12)
UONGOZI MIKOANI NA WILAYANI
Ili kufikia dhamira hiyo, chama Makao Makuu hakina budi kuueneza na kuusimamia U-Skauti nchini kote. Hili linatekelezwa na kwa Kamishna Mkuu na wawakilishi wake Mikoani na Wilayani.
Kwa mujibu wa Katiba ya Chama cha Skauti Tanzania ya mwaka 1997 Kifungu 6.11 (a) na (b) hawa watamwakilisha Kamishna Mkuu na kuyatekeleza majukumu yao ambayo kimsingi sawa na ya Kamishna Mkuu bali katika himaya zao.
Kwa mujibu wa Katiba ya Chama cha Skauti Tanzania kifungu 6.5 (e)(vi), Kamishna Mkuu amewateuwa viongozi wa Skauti wafuatao kuwa Makamishna wa Skauti wa Mikoa na wasaidizi wao:-
MKOA: Arusha
Kamishna: Shakirhussein Badruddin
Naibu Kamishna wake: Wilfred James
MKOA: Dar Es Salaam
Kamishna: Abubakari Mtitu
Naibu Kamishna wake: Grace Kado
MKOA:Dodoma
Kamishna: Daktari Swai
Naibu Kamishna wake: Selistine Raphael
MKOA:Geita
Kamishna: Kiracha Nyamsongolo
Naibu Kamishna wake: Marison .S. Gunje
MKOA: Iringa
Kamishna: John Sichone
Naibu Kamishna wake: Lyason Kajembura
MKOA:Kagera
Kamishna: Fr. Process Mutungi
Naibu Kamishna wake: Beda Kyaishozi
MKOA:Katavi
Kamishna: Mrisho Thabiti Kinanda
Naibu Kamishna wake: Selestine Yoachim China
MKOA: Kigoma
Kamishna: Doecles .H. Bigilwa
Naibu Kamishna wake: Eliudi Marwa
MKOA:Kilimanjaro
Kamishna: Hashim Nyari
Naibu Kamishna wake: Habibu .D. Mvungi
MKOA: Lindi
Kamishna: Aloyce Maira
Naibu Kamishna wake: Bakari Kayombo
MKOA: Mara
Kamishna: Yohana Bonyo
Naibu Kamishna wake: Fred Keya
MKOA: Manyara
Kamishna: Basilisa Martin
Naibu Kamishna wake: Khalifa Salehe Mfanya
MKOA: Morogoro
Kamishna: Francis .G. Francis
Naibu Kamishna wake: Mary Mpasa
MKOA: Mtwara
Kamishna: Erasto Nakati
Naibu Kamishna wake: Hassan .M. Mmadi
MKOA: Mbeya
Kamishna: Sadock Ntole
Naibu Kamishna wake: Boniface Dionis
MKOA: Mwanza
Kamishna: Elibarik Mmari
Naibu Kamishna wake: Wande Mwankyara
MKOA:Njombe
Kamishna: Tusiwene Mahenge
Naibu Kamishna wake: Anita Ngole
MKOA: Pwani
Kamishna: Musiba Bebusiba
Naibu Kamishna wake: Esto Joseph Kalale
MKOA: Rukwa
Kamishna: Mohamed Lugoya
Naibu Kamishna wake: Adengula Mwacha
MKOA: Ruvuma
Kamishna: S. .K. Ndunguru
Naibu Kamishna wake: Hamza Basil Bora
MKOA: Simiyu
Kamishna: Kulwa Mtebe
Naibu Kamishna wake: Jumanne Mangoli
MKOA: Shinyanga
Kamishna: Mussa Chama
Naibu Kamishna wake: Peter mgalula
MKOA: Tabora
Kamishna: Erick Nkwera
Naibu Kamishna wake: Kashinde Masamalo
MKOA:Tanga
Kamishna: Lt. Col (Mstaafu) John Mhina
Naibu Kamishna wake: Nassoro Mbajo
MKOA: Singida
Kamishna: Emmanuel Machemba
Naibu Kamishna wake: Juma SabigoroUTENDAJI
Kufuatia uteuzi wa Makamishna hao, taratibu za kuwaapisha na kuwakabidhi waranti na Katiba zitafuata hivi punde. Barua za uteuzi wao zinafuata. Wakati yote haya yanasubiriwa kwa taarifa hii ni ruksa kwao kuanza kazi mara moja. Alisema Mheshimiwa Shah.
MAKAMISHNA WA SKAUTI TANZANIA VISIWANI NA WILAYA
Mheshimiwa Shah aliendelea kusema, " Kauli mbiu ya Mkutano Mkuu Maalum wa uchaguzi ilikuwa 'UONGOZI IMARA, CHAMA IMARA' alifafanua kuwa, Chama cha Skauti hakina budi kuwa na uongozi imara unaoweza kusimamia maadili ya vijana wetu hapa nchini kuanzia Makao Makuu hadi Vijijini. Ni matarajio ya wadau wote wa Chama cha Skauti Tanzania kwamba viongozi wote waliochaguliwa, walioteuliwa na watakaoteuliwa wataongoza kwa kuzingatia Katiba na Maadili ya Chama. Aidha wito unatolewa kwa wanachama na marafiki wa Skauti kutoa ushirikiano kwa uongozi uliopo madarakani.
Kamishna Mkuu alimaliza kwa kuwashukuru wanahabari kwa ushirikiano wao.
MKUTANO WA 7 WA MUUNGANO WA WABUNGE SKAUTI DUNIANI
Mwenyekiti wa Umoja wa Skauti Wabunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Abdulkarim Ismail Shah amechaguliwa kuwa Mweka Hazina Mkuu wa Umoja wa Wabunge Skauti wa Dunia (WPSU)
walishiriki katika Mkutano Mkuu wa Sita wa Umoja wa Skauti Wabunge Duniani ambao unajumla ya nchi wanachama zaidi ya 50. Mkutano huo ulifanyika sambamba na uchaguzi wa viongozi wapya, uliofanyika mjini Tokyo Japan kuanzia Novemba Sita hadi Novemba Nane mwaka huu ambapo Tanzania iliwakilishwa na Mheshimiwa Shah na wabunge wengine watano pamoja na Katibu wa Bunge Umoja wa Wabunge Skauti Tanzania ndugu James John Warburg.
Wabunge wengine waliokuwemo kwenye ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano huo ni Mhe. Gosbert Blandes, Mhe Livingstone Lusinde, Mhe. kuruthum Mchuchuli na Mhe. Lucy Mayenga ambaye ni Makamo Mwenyekiti wa Umoja wa Skauti Wabunge wa Tanzania.
Katika uchaguzi huo ndugu Ryu Shionoya wa Japan amechaguliwa kuwa Rais mpya wa Umoja huo, na makamo wa kwanza wa Rais ni Bi. Ewa thalen Finne kutoka Sweden na makamo wa Rais wa pili ni ndugu Sutham Phanthusak kutoka Thailand.
Akizungumza na wandishi wa habari katikauwanja wa kimataifa wa ndege wa Mwalim Julius Kambarange Nyerere mara baada ya kuwasili kutoka japan, Mheshimiwa Shah amewashukuru wabunge wenzake kwa kumpigiania hadi kushinda kwenye nyadhifa hizo kubwa duniani na kwamba ushindi alioupata ni zawadi kwa Watanzania wote.
Amesema kuchaguliwa kwake kwenye nafasi hiyo ni heshima kwa Tanzania na kwamba ni ushindi kwa Tanzania na kuonyesha kuwa Tanzania inaweza kutoa viongozi katika kuongoza mashirika au taasisi mbalimbali Ulimwenguni, pia mbunge Mvumi Mtera Mhe. Lusinde alisisitiza kuwa ushindi huo pia umechangiwa na amani iliyopo Tanzania na kwa ushindi huo Tanzania imetangazika katika sekta ya Utalii na kujulikana kijiografia. Aliendelea kusema, "Uchaguzi huo uliohusisha mataifa zaidi ya 50 ulitawaliwa na ushindani mkali, lakini mgombea wa Tanzania alijieleza kwa ufasaha zaidi na vizuri kuwashawishi wajumnbe kumpigia kura na kushinda nafasi hizo.
Mkutano huo mkuu pia ulijadili na kupitisha mabadiliko ya Katiba ambapo muda wa kufanya mkiutano huo umeongezeka kutoka miaka mitatu hadi miaka minne.
Aidha kwamba kuwepo kwenye safu mpya ya uongozi wa Umoja wa Wabunge Skauti wa Dunia utamwezesha kuendeleza vijana kwa kuwapa elimu, ujuzi ili waweze kuajiliriwa au kujiajiri kwa ajili ya maendeleo yao wenyewe na kuondokana na umasikini. Alisema Mhe Shah.
Mbunge wa Karangwe Mhe. Gosbert Blandes amesema kwamba mkutano huo umemalizika kwa mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kujifunza namna vyama vya Skauti vinavyoendeshwa duniani, ameendelea kusema kuwa 'nchi nyingi duniani wanachukulia Skauti kama chanzo cha elimu na ajira kwa vijana hivyo wao kama wabunge wataishawishi Serikali kutenga fedha za kutosha kwa ajili ya kusaidia uendeshaji wa shughuli za Skauti nchini.
Wakati huo huo Mkutano wa tisa wa wabunge Skauti duniani unatarajia kufanyika nchini Tanzania katika kipindi cha miaka minne ijayo.
Kikubwa yaliyozungumziwa katika mkutano huo ni:

- Umuhimu wa kuweka mazingira salama kwa watoto kielimu.
- Umuhimu wa kuwaandaa na kuwapa fursa vijana kuwa viongozi wa baadaye.
- Majukumu mbalimbali ambayo Wabunge wanaweza kuyatekeleza kwa ajili ya kuwasaidia vijana na Chama cha Skauti.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)