Jumamosi, 18 Januari 2014

KAMATI YA UENDESHAJI YA MKOA YATEMA CHECHE


 Kuandaa Siku ya kumbukumbu ya Mwanzilishi wa Skauti Duniani

Mwenyekiti wa kikao cha Kamati ya Uendeshaji Mkoa wa Dar Es Salaam (aliyekaa mbele) Kamishna Abubakar Mtitu akiongoza ajenda katika kikao cha kamati hiyo tarehe 18 Januari katika Mgahawa Upanga Dar Es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Uendeshaji Mkoa wa Dar Es Salaam wakijadili ajenda katika kikao tarehe 18 Januari katika Mgahawa Upanga Dar Es Salaam.
Wa kwanza kushoto ni Mwanyato James, Titto Jackson, Bi Ramadevi na Naibu Kamishna Mkoa wa Dar Es Salaam Bi Grace Kado.

Chama cha Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam kupitia Kikao chake cha Kamati ya uendeshaji kimetoa wito kwa Skauti Mkoa wa Dar es Salaam kujiandaa na siku ya kumbukumbu ya mwanzilishi wa Skauti Duniani (Founder's Day) inayotarajiwa kufanyika kimkoa kuanzia tarehe 21 Februari, 2014 mpaka 23 Februari, 2014.
 
Kamishna wa Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam Ndugu Abubakar Mtitu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kikao cha kamati Uendeshaji cha Mkoa wa Dar Es Salaam, katika kiwanja cha Makao Makuu ya Skauti Upanga tarehe 18 Januari, 2014

"Wito unatolewa kufanya kazi za huduma kwa jamii kwa kujitolea kama ilivyo ada na wajibu wa Skauti" alisema Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Kamishna wa Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam Kamishna Abubakar Mtitu. Ndugu Mtitu alisisitiza kuwa Skauti ni watu wenye nidhamu, kujali na kufuata misingi ya utu, kujitoa kwa jamii katika kutekeleza kanuni na ahadi za Skauti.

Pia Kamishna Mtitu alisema mambo waliojadiliana katika kikao hicho ni muhimu sana katika kuendeleza Skauti na wanakamati wamekubaliana kutekeleza maazimio ya kikao hicho.



Mratibu Mafunzo wa Skauti 
Mkoa wa Dar Es Salaam
Ndugu Mwanyato James
Mwanyato James ambaye ni Mratibu wa Mafunzo Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam alisema katika mahojiano na waandishi wa habari kuwa "Natumai tutayatimiza yote tuliyoyajadili, pia nafuraha sana kuona kikao hiki kimehudhuliwa na watendaji wakuu wote wa Skauti Wilaya za Dar Es Salaam, naomba tuendelee hivi kwa kasi hii kwa maendeleo ya Skauti na jamii yetu"

Kamati imekubaliana kuandaa siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa Skauti Duniani (Founder's Day), Marehemu Paden Pawell aliyezaliwa tarehe 12 Februari 1857 na kufariki tarehe 8 Januari, 1941.

Mwenyekiti Mtitu alitumia fursa katika kikao hicho kuwatambulisha baadhi ya wajumbe wapya ambao ni James Mwanyato (Mafunzo), Mama Ramadevi Sankran Lyer (Kabu), Sameer Somji (Kazi Maalum), Titto Jackson pamoja na Leonard Gerlad Kiloka (Uakilishi wa Vijana) na wengine ni S. Salim (Mambo ya Nje na uhusiano), Reuben Mlay (Vijana), Anthony Meda (Makambi na Mawasiliano) na Bi Annick Verstraelen (Miradi)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni