Ijumaa, 20 Februari 2015

SEMINA ELEKEZI KWA TANZANIA NZIMA


  • Kuipa mafanikio makubwa Skauti
  • Cheche za mabadiliko zazidi kuonekana


Harakati za kuendeleza maendeleo ya kweli na kurudisha heshima ya Skauti kwa jamii,  harakati hizo zinazidi kukua na kuonekana zaidi, hii ni kufuatia utekelezaji ulio na weledi kwa viongozi wa Chama cha Skauti na Maskauti wote Tanzania.

Chama cha Skauti Tanzania kimeandaa semina elekezi kwa makamishna wote Tanzania, semina hiyo ya siku tatu kuanzia tarehe 18.02.2015 hadi 20.02.2015 inayoendelea katika ukumbi wa Don Bosco, Upanga jijini Dar Es Salaam.

Katika mahojiano na Dar Scout Habari Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania Mheshimiwa Abdulkarim Shah (Mb) alisema, ''Tumekutana kwa mujibu wa taratibu zetu za Skauti, na kwakuwa toka tumeteuliwa hatujawai kukutana na kufahamiana na pia kupanga mikakati ya pamoja katika kuhakikisha kwamba Skauti inafanya kazi zile zinazotakiwa kwa mujibu ya Katiba yetu na kanuni zake na pia kuisambaza Skauti nchini kote, isambae kwa manufaa ya vizazi na nchi yetu''.

Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania Mhe. Abdurkarim Ismail Shah (Mb) akiongea wakati wa ufunguzi wa Semina elekezi iliyofanyika katika ukumbi wa Don Bosco Upanga, Jijini Dar Es Salaam, tarehe 18.02.2015. Wakwanza kulia (walio kaa) ni Naibu Kamishna Mkuu Skauta Rashid Mchatta, akifuatiwa na Kamishna Mkuu Msaidizi kitengo cha Maafa, Majanga na Uhokoaji Skauta Juma Massudi na Kamishna Mkuu Msaidizi kitengo cha Miradi na Maendeleo Skauta Hamis Kerenge Masasa (aliyevaa furana nyeupe na miwani) wa kwanza kulia aliyesimama ni kamishna Mtendaji Ms. Eline Kitaly.
Na wa kwanza kushoto Kamishna Mkuu Msaidizi kitengo cha Utunzaji na Mazingira (aliyevaa nguo ya bluu) 

Mhe. Shah (Mb) aliendelea kusema, ''Kukutana kwetu hapa, mada mbalimbali zitatolewa na kupata fursa ya kuhoji na kutoa mawazo ambayo yote kwa pamoja yatawekwa katika mkakati wetu wa miaka minne na tunaamini kwamba kila mmoja atawajibika kwa nafasi yake kwa mujibu wa taratibu za Skauti'' aliendelea kusisitiza kwamba, ''Ili ndiyo kubwa kwa maana mafunzo yatakayo tolewa hapa tunahitaji kila mmoja wao aende kwa nafasi yake akawajibike''.


Kamishna Mkuu Mhe. Shah alieleza pia, viongozi hao watajengewa uwezo wa kufahamu pale linapotokea jambo hatua gani ichukuliwe ya ziada na kila jambo linalofanyika liweze kuratibiwa na kufika Makao Mkuu na kuwepo na taarifa hizo, pamoja na Skauti kujua na kuwa na taarifa moja ya kila jambo, kuanzia za kambi na nyinginezo. Hii ni faida kubwa ya utawala bora.


Wajumbe wa Semina Elekezi wakisikiliza jambo kwa makini wakati Kamishna wa Mkoa wa Dar Es Salaam Abubakar Mtitu (aliye simama aliyevaa furana ya zambarau) akichangia mada katika semina hiyo, siku ya tarehe 18.02.2015 katika ukumbi wa Don Bosco Upanga, jijini Dar Es Salaam.

Elasto Nangati Kamishna wa Mkoa wa Mtwara alisema, ''Semina hii Elekezi itawawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi, ukizingatia hatujawai kupewa semina elekezi kama hii kwa hiyo mabadiliko yatakuwepo sana baada ya semina hii''. Aliendelea kusema kuwa, ''Lengo ni kuboresha utaratibu wa uendeshaji, inamanufaa kwangu na kwa wenzangu, kwani itatujengea uwezo sana wa kazi''


Kamishna Mkuu Msaidizi kitengo cha Miradi na Maendeleo Skauta Hamis Kerenge Masasa (aliyesimama) akiwaelekeza jambo wana semina.

Katika semina hii Skauti zaidi ya 112 wa jinsi zote walihudhuria, katika hali iliyokuwa nzuri ya upendo na viongozi hao walionekana kuvalia sare za kila aina na huku wakiwa na nyuso za furaha.

Kiongozi kutoka Tanzania Zanzibar Skauta Makame Ali alisema, ''kulikuwa na vitu ambapo tulikuwa kama kwenye giza kwa sasa tumefunuliwa na kujua mengi, nami nitaenda kuwaelekeza wenzangu pindi nitakaporudi''.






Makamishna wakiwa katika kazi za vikundi katika Semina Elekezi

Skauti walipata fursa ya kufundishwa mchezo wa CHESS



Tembelea: twitter @DarScout 

facebook Dar Es Salaam Scout

Jisajiri kwa habari mbali mbali za Skauti (Scout Breaking News)
na Scout Chat 0655-095559


TANZIA


ALIYEKUWA MWEKA HAZINA WA SKAUTI MKOA WA DAR ES SALAAM AFARIKI DUNIA.

Akiongea na Dar Scout Habari kwa njia ya simu ya kiganjani Kamishna wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Abubakar Mtitu alisema, ''Skauti tumepatwa na msiba, aliyekuwa Mweka Hazina wa Skauti Mkoa wa Dar amefariki dunia usiku wa tarehe 18.02.2015''

Kamishna Mtitu aliendelea kusema uku sauti yake ikisikika kuwa na majonzi, ''Hivi karibuni marehemu alitakiwa kupelekwa nchini India kwa ajili ya matibabu, lakini sasa hatuaye tena''.

Hata hivyo Dar Scout Habari ilishindwa kupata jina la marehemu na alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa gani, kwani mawasiliano yalikuwa mabaya yalikatika na mpaka tunapoenda mtamboni hatukuweza kufanikiwa kumpata tena kwa njia ya simu kamishna wa mkoa na viongozi wa mkoa huo kwa kupata habari zaidi.

Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa tarehe 20.02.2015 kuelekea Kagera kwa mazishi, na msiba upo nyumbani kwa marehemu Kiwarani, jijini Dar Es Salaam. Hakika mbele ya haki ametutangulia, Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema, Amina.

Jumanne, 10 Februari 2015

SHEREHE ZA KUMBUKUMBU YA MWANZILISHI WA SKAUTI 2015

  • MAANDALIZI YAKAMILIKA KWA ASILIMIA 90
  • JK KUWA MGENI RASMI
 
Chama cha Skauti Tanzania kupitia Kamishina Mtendaji Bi. Eline Kitaly katika taarifa yake kwa njia ya barua pepe kwa Kamishina wa Skauti wa mkoa wa Dar Es Salaam na Kamishina wa Wilaya pamoja na wasaidizi wao (nakala ya barua pepe hiyo DarScout Habari inayo) imesema kuwa maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa na kuwataka kuhamasisha Skauti wao kuhudhuria kwa wingi pamoja na kulipia ada ya uanachama na kukamilisha taratibu zote za "Smart Card".
 


Maandalizi ya Kumbukumbu ya Mwanzilishi wa Skauti Duniani kwa mwaka 2015 yameandaliwa na Makao Makuu kwa kushirikiana na Skauti Mkoa wa Dar es Salaam, yatakuwa ya aina tofauti na ya kipekee zaidi. Wakizungumza na chombo hiki cha habari cha Dar Scout Habari kwa nyakati tofauti, Kamishna wa Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam, Skauta Abubakari Mtitu alisema, "Tumekwisha kamilisha jukumu letu na matayarisho yanaenda vizuri zaidi"
 
Abubakari Mtitu
Kamishna wa Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam

Naye Kamishna Mkuu Msaidizi wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kimataifa, Habari na JotaJoti, Skauta Fredrick Nguma alibainisha kwa kusema, "Mwaka huu katika maazimisho ya kumbukumbu za mwanzilishi wa Skauti duniani, mgeni rasmi atakuwa Mlezi wa chama chetu ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Prof. Jakaya Mrisho kikwete, na maazimisho hayo yatafanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar Es Salaam"


Fredrick Peter Nguma
Kamishna Mkuu Msaidizi wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa kimataifa, Habari na JotaJoti
 

"Katika kuelekea kuazimisha kumbukumbu hiyo, Wito unatolewa kufanya kazi za huduma kwa jamii kwa kujitolea kama ilivyo ada na wajibu wa Skauti" ulisema mtandao USIO RASMI wa WhatsApp wa "Scout Chat - SC". Mtandao huo ulisisitiza kuwa Skauti ni watu wenye nidhamu, kujali na kufuata misingi ya utu, kujitoa kwa jamii katika kutekeleza kanuni na ahadi za Skauti.

Pia majadiliano katika mtandao ambao unazidi kuwa maarufu katika chama na February 02, 2015 umetimiza mwaka mmoja toka uanzishwe, ulisisitiza kuwa mambo wanayoyajadili viongozi katika kikao cha maandalizi ni muhimu sana katika kuendeleza Skauti na wajumbe wa "Scout Chat" wamekubaliana kutekeleza maazimio ya kamati hiyo ya maandalizi.

 

 
 
 Jiunge na Dar Scout Habari:  Scout Chat (SC) WhatsApp +255-655-095559