|
Baadhi ya Skauti wakisikiliza maelekezo toka kwa mmoja wa afisa wa ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Arusha (AICC) |
Ni desturi ama kawaida ya Skauti ulimwenguni kufanya ziara za mafunzo kwa ajili ya elimu na kuwajengea ujasiri, mafunzo hayo ufanywa kwa kutembelea sehemu mbalimbali za kihistoria, jiografia, kisayansi na mengineyo. Mwezi wa Desemba 2012, Skauti mkoa wa Dar Es Salaam walifanya mafuanzo hayo kwa kufanya utalii wa ndani, kujifundisha jiografia, historia na mengineyo kwa kutembelea eneo la hifadhi ya Ngorongoro, ukumbi wa mikutano ya kimataifa wa Arusha (AICC).
Pamoja na kutembelea hifadhi ya taifa, waliweza kujifunza maisha ya nyoka, wanavyoishi na kuzaliana, kuona na kujifunza maisha ya wanyama, ndege na wadudu. Kujifunza mila na desturi za kabila la Wamasaai, na jinsi gani wanavyoweza kuishi katika hifadhi ya wanyama bila madhara yoyote na kuendeleza kutunza mazingira.
|
Baadhi ya Skauti wakiwa wamevaa nguo za Kimasaai |
|
Kamishina wa Skauti wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Abubakari Mtitu (aliye vaa furana) akiwa na baadhi ya Skauti waliovaa vazi la Kimasaai katika mafunzo ya kielimu Ngorongoro Desemba 2012 |
|
Skauti wakiwa wamepanda Ngamia Mkoani Arusha katika ziara ya Kielimu na Ujasiri katika Hifadhi ya Taifa ya wanyama Ngorongoro. |
|
Skauti wakiangalia bonde la hifadhi ya Ngorongoro |
Ziara nyingine ilikuwa Hong Kong, uko Skauti waliweza kutembelea chuo cha mafunzo cha Skauti wa majini (Pak Sha Wan " Sea activity training block) wa mji wa Hong Kong nchini China pamoja na "DREAM ISLAND".
|
Baadhi ya Skauti wa Mkoa wa Dar Es Salaam wakiwa katika chuo cha mafunzo cha Skauti wa majini Hong Kong Desemba 2012 wakipata maelekezo. |
|
Skauti wakiwa wanaangalia mandhali karibu na chuo cha Skauti wa majini (baharini) Hong Kong walipokwenda katika ziara ya mafunzo ya Kielimu na Ujasiri, wa mbele kushoto alivaa sare ni Juma Massudi kulia ni Skauti wa Hong Kong mwenyeji wao na nyuma aliyevaa shati jeupe na mistari ya viboksi ni Faustin Magige viongozi wa ziara hiyo, Desemba 2012. |