Jumatano, 23 Mei 2012

Mwenge wa Uhuru

SKAUTI WILAYA YA ILALA WASHIRIKI KUUPOKEA MWENGE WA UHURU
Skauti wilaya ya Ilala wakiwa pamoja na wakimbiza Mwenge katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kutoka wilaya ya Temeke kwenda wilaya ya Ilala tarehe 26/06/2012 eneo la Stesheni ya TaZara, Dar Es Salaam.
 Skauti wilaya ya Iala wakiwavisha skafu wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa katika viwanja vya Stesheni ya TaZara, Dar Es Salaam.
 Mkuu wa wilaya ya Temeke Mh. Sophia Mjema akimkabidhi Mwenge wa Uhuru mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Raymond Mushi tarehe 26/06/2012 katika eneo la Stesheni ya TaZara, Dar Es Salaam.



SKAUTI WILAYA YA ILALA WAENDESHA MAFUNZO YA UONGOZI WA KIKOSI  
PATROL LEADER COURSE- (PEER EDUCATOR TRAINING)
Wahitimu wa mafunzo ya uongozi wa kikosi wilaya ya Ilala wakionyesha vyeti vyao baada ya kuhitimu mafunzo hayo katika viwanja vya makao makuu ya Skauti Dar Es Salaam. Mafunzo hayo yalianza tarehe 22/06/2012 mpaka 24/06/2012.
Kamishina wa Skauti Mkoa wa Dar-Es-Salaam Abubakar Mtitu (aliyevaa fulana ya mistari) akiwapa maelekezo ya mchezo wa kuonyesha umuhimu wa kutunza kumbukumbu washiriki wa mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo wakisikiliza jambo
Baadhi ya washiriki wa mafunzo wakiwa katika hema wakibadilishana mawazo juu ya mafunzo ya uongozi wa kikosi
 Scouts Life Saving Activity

 
Sherehe ya kuapishwa kwa Skauti Mkuu Kanali mstaafu .O. Kipingu Ikulu jijini Dar es Salaam, mwaka 2008.
Mlezi  wa Skauti Tanzania Mhe. Dkt Jakaya .M. Kikwete (Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (aliyevaa suti nyeusi). Wa kwanza kulia ni Makamo wa Rais Tanzania Mhe. Ali .M. Shein, [kulia kwa rais ni mkufunzi wa Chama cha Skauti Tanzania ndugu Ngunga.


Naibu Waziri wa Elimu, Mhe. Mwantumu Mahiza aliyevaa kofia ya kijani akibadilishana mawazo na wajumbe wa mkutano wa Skauti wa nchi za Afrika Mashariki mjini Morogoro katika kambi ya Bahati, mwaka 2008.