MAKAMISHNA WA SKAUTI MIKOA NA NAIBU WAO WAAPISHWA
Sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mwasisi wa Skauti Duniani Marehemu Baden-Powell zimefanyika katika nchi mbalimbali za Dunia.
Katika Jiji la Dar Es Salaam Sherehe hizo zilifanyika katika Kiwanja cha Kimataifa cha Biashara cha Mwalim Julius Kambarage Nyerere (Saba-Saba) barabara ya kilwa.
Shughuli hiyo iliyoandaliwa na Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam kwa kamati iliyoongozwa na Kamishna wa Skauti wa Mkoa huo Ndugu Abubakar Mtitu.
Katika sherehe hiyo, Kamishna Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania (TSA) ndugu Abdulkarim Ismail Shah aliwaapisha Kamishna wa Mikoa na Manaibu wake.
Pia katika sherehe hiyo chama cha Skauti Tanzania kilizindua Mpango Mkakati wa Chama hicho.
Mgeni wa rasmi katika Sherehe hiyo alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Ufundi Stadi Bi. Consolata Mgimba kwa niaba ya Rais wa Chama ambaye ni Waziri wa Elimu na Mafunzo Mheshimiwa Shukuru Kawambwa alifika katika eneo la sherehe mnamo saa nne asubuhi tayari kwa kupokea maanamano na kuaza kwa sherehe hiyo.
Mgeni rasmi Bi. Consolata Mgimba Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Ufundi akivishwa Skafu na Skauti tayari kupokea maandamano ya Skauti, tarehe 22 Februari 2014 |
Mgeni rasmi Bi. Consolata Mgimba Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Ufundi akitoa salamu kwa niaba ya Rais wa Chama ambaye ni Waziri wa Elimu na Mafunzo Mheshimiwa Shukuru Kawambwa |